• HABARI MPYA

    Friday, June 22, 2018

    CHRISTIAN BELLA KUTUMBUIZA MAREKANI JUNI 30 KATIKA USIKU WA UTAMADUNI WA MSWAHILI

    Na Mahmoud Zubeiry, MARYLAND
    MWANAMUZIKI maarufu nchini Tanzania, Christian Bella mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) anatarajiwa kutumbuiza kwenye Usiku wa Utamaduni wa Mswahili kwenye ukumbi wa Hampton Inn 9670, Baltimore Avanue, Maryland 20740 Juni 30, mwaka huu mjini Maryland, Marekani.
    Onyesho hilo limeandaliwa na Mtangazaji maarufu wa zamani wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), tangu enzi za Radio Tanzania (RTD), Steven Mgaza ambaye pia kwa hapa Marekani ametangazia kwa muda mrefu Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika (VoA).
    Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online mjini hapa leo, Mgaza amesema kwamba maandalizi ya onyesho hilo yamekamilika na kwa sasa wanajiandaa kumpokea Bella na wenzake.

    Christian Bella anatarajiwa kutumbuiza kwenye Usiku wa Utamaduni wa Mswahili nchini  Marekani Juni 30, mwaka huu

    “Ni tamasha maalum la kuutangaza utamaduni wa Kiswahili huku Marekani na siku hiyo kutakuwa na mambo mbalimbali ya asili ya Kiswahili, kwa ujumla ni raha za Pwani, mavazi, vyakula na ngoma za asili,”amesema Mgaza.
    Pamoja na hayo, Mgaza amesema kwamba siku hiyo pia kutakuwa na ngoma za asili na burudani nyingine mbalimbali ambazo moja kwa moja zitakuwa zinautangaza uswahili.   
    Bella, kijana kutoka DRC kwa sasa anatamba na bendi yake ya Malaika baada ya kuletwa nchini na bendi ya Akudo mwaka 2005.
    Na nyimbo zake maarufu ni pamoja na Yako Wapi Mapenzi, Ameondoka zilizompatia umaarufu akiwa na Akudo kabla ya kuanzisha bendi yake, Malaika na kutoa vibao vingine vikali kama Nani Kama Mama na Amerudi Analia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHRISTIAN BELLA KUTUMBUIZA MAREKANI JUNI 30 KATIKA USIKU WA UTAMADUNI WA MSWAHILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top