• HABARI MPYA

  Thursday, June 21, 2018

  BIASHARA UNITED YASAJILI WACHEZAJI WANNE WA KIGENI

  Na Mwandishi Wetu, MARA
  UONGOZI wa timu ya Biashara United Mara imetambulisha wachezaji wanne raia wa kigeni kutoka Mataifa manne barani Afrika.
  Meneja wa timu hiyo Aman Josiah amesema lengo kubwa ni kuimarisha kikosi cha timu hiyo pamoja na wachezaji waliopandisha timu hiyo kutoka daraja la kwanza ili kuwa na ushiriki mzuri wa ligi kuu Tanzania Bara msimu wa 2018/2019.
  Wachezaji hao ni Balora Nouridine, golikipa kutoka Burkina Faso, Alex Olumide, kiungo kutoka Nigeria, Wilfried Kourouma, kiungo kutoka Guinea na Astin Amos, mshambuliaji kutoka Ivory Coast ingawa alikuwa anacheza Qatar.


  Hata hivyo, meneja huyo amesema bado wataendelea kuimarisha kikosi hicho na kuhakikisha kinaleta ushindani mkubwa katika ligi kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BIASHARA UNITED YASAJILI WACHEZAJI WANNE WA KIGENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top