• HABARI MPYA

    Sunday, June 24, 2018

    RAZA AJITOKEZA KUUTAKA URAIS WA ZFA ILIYOGUBIKWA NA MIGOGORO

    Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
    MWAKILISHI wa jimbo la Uzini Mohammed Raza Hassanal ametangaza nia ya kugombea Urais wa Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA) kwa ajili ya kurejesha hadhi ya soka visiwani hapa.
    Raza ameyasema hayo wakati akizungumza na wandishi wa habari za michezo katika hafla maalum iliyofanyika katika ukumbi wa hotel ya Golden Tulip Malindi Mjini Unguja.
    Mwanamichezo huyo ambae aliwahi kuwa mshauri wa masuala ya michezo kwa Rais wa awamu ya tano Dk Salmin Amour, amesema nia hiyo imekuja baada ya kuona soka la Zanzibar kuanguka, hivyo ameona ipo haja kutangaza nia ili kuja kulikomboa.

    Mohammed Raza (kulia) ametangaza nia ya kugombea Urais wa ZFA ili kurejesha hadhi ya soka ya Zanzibar 

    Amesema atahakikisha anaukuza mchezo huo kwani atashirikiana ipasavyo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo inaonekana ipo mstari wa mbele kwenye michezo.
    ZFA watalazimika kufanya uchaguzi kufuatia viongozi wake wakuu kuamua kujiuzulu akiwemo aliyekuwa Rais Ravia Idarous Faina, Makamo Urais ZFA Pemba Ali Mohammed Ali na Makamo Urais ZFA Unguja Mzee Zam Ali hivyo nafasi hizo mpaka sasa zipo tupu huku ikisubiriwa kamati ya Uchaguzi kutangaza tarehe za kuanza harakati za kufanyika uchaguzi huo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RAZA AJITOKEZA KUUTAKA URAIS WA ZFA ILIYOGUBIKWA NA MIGOGORO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top