• HABARI MPYA

    Thursday, June 28, 2018

    SIMBA YAWATAMBULISHA RASMI WAWA, KAGERE NA DIDA

    Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM
    MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba leo wamewatambulisha wachezaji wake watatu wapya ambao watawatumia katika michuano iliyo mbele yao ikiwemo Kombe la Kagame litakaloanza kesho.
    Wachezaji waliotambulishwa leo na Simba mbele ya waandishi wa habari ni Serge Wawa Pascal 'Ramos', Mohammed ‘Meddie’ Kagere kutoka Gor Mahia na Deogratius Munishi ‘Dida’ kutoka Pretoria University ya Afrika Kusini.
    Akiwatangaza wachezaji hao, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema nyota hao wamesajiliwa kwa kuzingatia timu yao msimu ujao itashiriki michuano mingi.
    “Nawatangaza wachezaji hawa kwenu ili umma uweze kuwafahamu na hawa wamesajiliwa ili kuiongezea nguvu timu yetu msimu ujao. Tumemsajili Meddie, Dida na Wawa ili kuongeza upana wa kikosi chetu.

    Kaimu kocha Mkuu wa Simba, Masoud Juma kutoka Burundi akimkabidhi jezi Serge Wawa Pascal leo

    “Hatutaki kusajili watu wa maneno mengi, huyu Meddie wakati tunacheza mechi ya fainali kule Kenya tukiwa kwenye korido kabla ya kuingia uwanjani, niliongea maneno ya shombo ili kuwatoa mchezoni Gor Mahia.
    “Meddie aliniangalia tu, hakusema neno lolote lakini tulipoingia uwanjani akatufunga, huyu ndiye aina ya wachezaji tuwatakao,” alisema Manara.
    Manara pia alisema klabu imewasajili wachezaji wengine watatu ambao ni Marcel Kaheza kutoka Majimaji, Adama Salama kutoka Lipuli na Mohammed Rashida wa Prisons ya Mbeya. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA YAWATAMBULISHA RASMI WAWA, KAGERE NA DIDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top