• HABARI MPYA

  Sunday, July 23, 2017

  SIMBA YAMTOA KWA MKOPO MANYIKA AKAWE NAMBA 1

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  RASMI, Simba SC imesema itamtoa kwa mkopo kipa wake, Peter Manyika kwenda timu ambayo atapata nafasi ya kucheza kama chaguo la kwanza.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema leo kwamba, Manyika bado ana miaka miwili ya kuendelea kuwa mchezaji wa klabu hiyo kulingana na mkataba wake, lakini msimu ujao atacheza timu nyingine.
  Lengo la Simba ni kuokoa kipaji cha kipa huyo, mtoto kipa wa zamani wa kimataifa nchini, Manyika Peter aliyewika Yanga SC. Hata hivyo, Hans Poppe hajasema Manyika anakwenda timu gani.
  Peter Manyika anaondoka Simba kwenda kucheza kwa mkopo timu ambayo atakuwa chaguo la kwanza anusuru kipaji chake


  REKODI YA PETER MANYIKA SIMBA 

  Jumla ya mechi alizodaka: 51

  Mechi alizodaka bila kufungwa: 30

  Jumla ya mabao aliyofungwa: 34

  Pamoja na Manyika, Simba imeachana na kipa wake mwingine mdogo, Dennis Richard iliyempandisha kutoka timu B.
  Na Simba inaachana na makipa wake hao, baada ya kuwasajili kwa mpigo makipa namba moja na namba mbili wa timu ya taifa, Taifa Stars, Aishi Manula kutoka Azam FC na Said Mohammed kutoka Simba SC.  
  Manyika aliyesajiliwa Simba SC Julai mwaka 2014, amedaka jumla ya mechi 51 za mashindano tofauti, nyingi za kirafiki akifanikiwa kusimama langoni mara 30 bila kuruhusu nyavu zake kuguswa huku akiwa amefungwa jumla ya mabao 34.  
  Peter Manyika (kulia) akiwa na baba yake, Manyika Peter (kushoto)

  MECHI ALIZODKA MANYIKA SIMBA NA MATOKEO YAKE;
  Simba SC 0-0 Orlando Pirates (kirafiki aliingia dk43 hakufungwa, Afrika Kusini) 
  Simba SC 2-4 Bidvest Witss (Kirafiki, alifungwa nne Afrika Kusini) 
  Simba SC 0-2 Jomo Cossmos (Kirafiki, alifungwa mbili Afrika Kusini) 
  Simba SC 0-0 Yanga SC (Ligi Kuu, hakufungwa)
  Simba SC 1-1 Prisons (Ligi Kuu, alifungwa moja)
  Simba SC 1-1 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu, aliokoa penalty, akafungwa moja)
  Simba SC 0-0 Express (Kirafiki, hakufungwa) 
  Simba SC 0-1 Mtibwa Sugar (Kombe la Mapinduzi, Zanzibar alifungwa moja)
  Simba SC 1-0 Mafunzo (Kombe la Mapinduzi, Zanzibar hakufungwa)
  Simba SC 1-0 JKU (Kombe la Mapinduzi, hakufungwa)
  Simba SC 4-0 Taifa Jang’ombe (Robo Fainali Kombe la Mapinduzi, hakufungwa)
  Simba SC 1-0  Polisi (Nusu Fainali Kombe la Mapinduzi, hakufungwa)
  Simba SC 0-0  Mtibwa Sugar (Alimpisha Ivo dakika ya 90, Simba ikashinda penalti 4-3 Fainali Kombe la Mapinduzi)
  Simba SC 2-0 Ndanda FC (Ligi Kuu Mtwara, hakufungwa)
  Simba SC 1-1 Azam FC (Ligi Kuu, alifungwa moja) 
  Simba SC 1-2 Mbeya City (Ligi Kuu Taifa, alifungwa mbili)
  Simba SC 2-0 Polisi Moro (Ligi Kuu, aliingia kipindi cha kwanza kumalizia baada ya Ivo kuumia, hakufungwa) 
  Simba SC 0-2 Mgambo Shooting (Ligi Kuu, alifungwa moja baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Ivo aliyetolewa kwa kadi nyekundu kipindi cha pili)
  Simba SC 3-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu, hakufungwa)
  Simba SC 2-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu, aliungwa moja)
  Simba SC 3-0 Toto Africans (Kirafiki Mwanza, akiingia kipindi cha pili hakufungwa)
  Simba SC 0-2 Mbeya City (Alifungwa mbili, Ligi Kuu)
  Simba SC 2-1 Zanzibar Kombaini (Alifungwa moja, Kirafiki Zanzibar) 
  Simba SC 4-0 Black Sailor (Hakufungwa Kirafiki Zanzibar)
  Simba SC 3-2 KMKM (Alifungwa mbili, akatolewa kipindi cha piliKirafiki Zanzibar)
  Simba SC 2-1 URA (Alifungwa moja, kirafiki Taifa)
  Simba SC 0-0 Mwadui FC (Hakufungwa, kirafiki Dar alimpokea Dennis Richard)
  Simba SC 3-1 JKU (Alifungwa moja, Kirafiki Zanzibar)
  Simba SC 1-0 African Sports (Hakufungwa, Ligi Kuu Tanga)
  Simba SC 2-0 JKT Mgambo (Hakufungwa, Ligi Kuu Tanga)
  Simba SC 3-1 Kagera Sugar (Alifungwa moja, Ligi Kuu Taifa)
  Simba SC 0-2 Yanga SC (Alifungwa mbili, Ligi Kuu Bara)
  Simba SC 1-0 Stand United (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
  Simba SC 1-3 Geita Gold Mine (Alifungwa tatu Kirafiki Geita)
  Simba SC 2-2 Jamhuri FC (Alifungwa mbili, Kombe la Mapinduzi)
  Simba SC 1-0 URA FC (Hakufungwa, Kombe la Mapinduzi)
  Simba SC 1-0 JKU FC (Hakufungwa, Kombe la Mapinduzi)
  Simba SC 0-1 Mtibwa Sugar (Alifungwa moja, Nusu Fainali Kombe la Mapinduzi)
  Simba SC 3-0 Kombaini ya Meatu (Hakufungwa, hakumaliza Kirafiki, Bariadi, Shinyanga)
  Simba SC 3-0 Mafunzo (Hakufungwa, Kirafiki, Zanzibar) 
  Simba SC 0-0 Majimaji FC (Hakufungwa Ligi Kuu, Songea)
  Simba SC 1-0 Mtibwa Sugar (Hakufungwa Ligi Kuu, Morogoro)
  Simba SC 1-2 JKT Ruvu (Alifungwa mbili Ligi Kuu, Taifa)
  Simba 5-0 Burkina Faso (Hakufungwa Kirafiki Moro, alimaliza) 
  Simba 0-0 URA (Hakufungwa Kombe la Mapinduzi)
  Simba 2-0 Jang’ombe Boys (Hakufungwa Kombe la Mapinduzi)
  Simba SC 3-0 Polisi Dodoma (Hakufungwa kirafiki Jamhuri, Dodoma)
  Simba 1-0 Mererani Stars (Hakufungwa kirafiki Uwanja wa CCM Mererani, Arusha)
  Simba 7-0 Geita Gold Sports (Hakufungwa Kirafiki, Geita)
  Simba 3-2 Mbao FC (Alifungwa mbili Ligi Kuu Kirumba)
  Simba 2-0 Rhino Rangers (Hakufungwa Kirafiki Tabora)
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YAMTOA KWA MKOPO MANYIKA AKAWE NAMBA 1 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top