• HABARI MPYA

    Sunday, July 23, 2017

    PLUIJM AFUNGA USAJILI SINGIDA UNITED NA MKONGWE KIGI MAKASI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIUNGO anayeweza kucheza kama beki pia, Kigi Makasi, amekamilisha uhamisho wake kutoka Ndanda FC kujiunga na timu mpya katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Singida United FC kwa mkataba wa miaka miwili.
    Kocha Mkuu wa Singida United, Mholanzi Hans van der Pluijm amemkabidhi jezi Kigi leo aanze maisha mapya ya soka baada ya kuchezea Yanga, Simba na Ndanda FC.    
    Mtendaji Mkuu wa Singida United, Sanga Festo leo ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online kwamba Kiggi anafanya idadi ya wachezaji wa Singida United kufika 25, kati yao 16 wakiwa ni wapya waliosajiliwa kutoka timu mbalimbali, wakati tisa walikuwemo kwenye vita ya kupandisha timu Ligi Kuu kutoka Daraja la Kwanza.
    Kocha Mholanzi Hans van der Pluijm (kulia) akimkabidhi jezi ya Singida United, Kigi Makasi (kushoto) baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili 

    Sanga amesema wamepata mchezaji mzuri anayeongoza kwa moyo wa kujituma vilivyo uwanjani, Makasi ambaye ameamua kujivua beji ya Unahodha wa Ndanda FC na kuhamia katikati ya nchi ya Tanzania kuungana na timu ya Ushindi, SU.
    Ikumbukwe Singida United ilianza kwa kukamilisha usajili wa wachezaji saba wa kigeni kwa mujibu wa kanuni, ambao ni Elisha Muroiwa, Twafadzwa Kutinyu, Simbarashe Nhivi na Wisdom Mtasa wote kutoka Zimbabwe, Shafik Batambuze kutoka Uganda, Dany Usengimana na Michel Rusheshangoga kutoka Rwanda.
    Wachezaji wengine wapya wazawa mbali ya Kigi ni Atupele Green kutoka JKT Ruvu, Miraj Adam kutoka Africa Lyion, Kenny Ally kutoka Mbeya City, Roland Msonjo kutoka Mshikamano FC, Pastory Athanas kutoka Simba, Ally Mustafa ‘Barthez’, Deus Kaseke kutoka Yanga na Salum Chuku kutoka Toto Africa.
    “Tunawashukuru vilabu mbalimbali ambao tulifikia makubaliano nao na wamewachukua baadhi ya wachezaji wetu walioipandisha timu, na baadhi ya wachezaji waliomba kuondoka kwa ridhaa yao,”amesema Sanga.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PLUIJM AFUNGA USAJILI SINGIDA UNITED NA MKONGWE KIGI MAKASI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top