• HABARI MPYA

  Monday, July 24, 2017

  DE GEA APANGUA PENALTI MBILI, MAN UNITED YAIGONGA REAL KWA MATUTA

  MANCHESTER United imeifunga kwa penalti 2-1 Real Madrid katika mchezo wa Kombe la Mabingwa wa Kimataifa baada ya sare ya 1-1 usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Levi's mjini Santa Clara, California, Marekani.
  Shujaa wa Mashetani Wekundu, amekuwa ni kipa Mspaniola, David De Gea ambaye anatakiwa sana na Real Madrid ya nyumbani kwako, aliyeokoa penalti mbili za Mateo Kovacic na Oscar.
  Ni mikwaju mitatu tu ya penalti ilitinga nyavuni kati ya 10 iliyopigwa, huku matuta ya Man United yakifungwa na Daley Blind na Henrikh Mkhitaryan na ya Real ikifungwa na Luis Quezada.

  David De Gea akifurahia baada ya kuokoa za penalti za Real Madrid na kuipa ushindi Manchester United Marekani PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Wengine waliokosa penalti za Real Madrid ni Theo Hernendez na Casemiro, wakati upande wa United waliokosa ni Anthony Martial, Scott McTominay na Victor Lindelof.   
  Awali ya hapo, katika dakika 90 za mchezo, Jesse Lingard alianza kuifungia United dakika ya 45 na ushei akimalizia kazi nzuri ya Anthony Martial, kabla ya Casemiro kuisawazishia Real kwa penalti dakika ya 69 baada ya Victor Lindelof kumuangusha Theo Hernandez. 
  Kikosi cha Real Madrid kilikuwa; Navas, Carvajal/Hakimi dk46, Varane/Quezada dk46, Nacho/Manu dk46, Marcelo, Modric/Kovacic dk46, Kroos, Isco/Oscar dk46, Vazquez/Hernandez dk46, Benzema/Gomez dk46, Bale/Franchu dk46.
  Man United; Romero/De Gea dk46, Fosu-Mensah/Blind dk46, Bailly/Smalling dk46, Jones/Lindelof dk46, Darmian/Valencia dk77, Carrick/Pogba dk46, Lingard/Mkhitaryan dk46, Fellaini, A Pereira/Herrera dk46/McTominay dk52, Martial na Rashford/Lukaku dk46.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DE GEA APANGUA PENALTI MBILI, MAN UNITED YAIGONGA REAL KWA MATUTA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top