• HABARI MPYA

    Tuesday, July 18, 2017

    KAMUSOKO BADO ‘ANAVUTANA’ NA YANGA KUHUSU MKATABA MPYA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIUNGO Mzimbabwe, Thabani Scara Kamusoko bado anavutana na uongozi wa klabu hiyo juu ya mkataba mpya, kufuatia kumaliza wa awali wa miaka miaka miwili.
    Kamusoko ndiye mchezaji pekee hana uhakika wa kuendelea kuichezea Yanga msimu ujao kati ya waliokuwepo kwenye kikosi cha timu hiyo msimu uliopita, ambao wapo kwenye mipango ya kocha Mzambia George Lwandamina.
    Bin Zubeiry Sports – Online inafahamu kwamba mazungumzo baina ya Kamusoko aliyejiunga na Yanga mwaka juzi akitokea FC Platinums ya kwao, Zimbabwe na uongozi yanaendelea vizuri na wakati wowote pande hizo mbili zitatangaza ndoa yao mpya.
    Wachezaji wengine wote muhimu wakiwemo washambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa, Mzimbabwe Donald Ngoma na Mrundi, Amissi Tambwe.
    Thabani Kamusoko bado anavutana na uongozi wa klabu hiyo juu ya mkataba mpya, kufuatia kumaliza wa awali wa miaka miaka miwili

    Hata hivyo, kwa sasa ni wachezaji 16 tu ndiyo wapo mazoezini Yanga SC kwa sasa wakiendelea na maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, chini ya kocha Lwandamina.
    Hao ni pamoja wapya wanne, kipa Mcameroon, Youthe Rostand aliyesajiliwa kutoka African Lyon, beki Abdallah Hajji ‘Ninja’ kutoka Taifa Jang’ombe, kiungo Pius Buswita kutoka Mbao FC na mshambuliaji Ibrahim Ajib kutoka kwa mahasimu, Simba SC.
    Wengine ni mabeki, Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Juma Abdul, Pato Ngonyani, Mwinyi Hajji Mngwali, Andrew Vincent ‘Dante’, viungo Geoffrey Mwashiuya, Juma Mahadhi, Said Juma Makapu, Emmanuel Martin, Yussuf Mhilu, Obrey Chirwa na mshambuliaji Amissi Tambwe.
    Wachezaji ambao hawapo ni pamoja na majeruhi watatu, kipa Benno Kakolanya, kiungo Deus Kaseke na mshambuliaji Donald Ngoma.
    Beki Hassan Kessy na winga Simon Msuva wapo na kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars ambacho kesho kinakwenda Kigali, Rwanda kwa ajili ya mchezo wa marudiano na Rwanda mwisjoni mwa wiki kuwnaia tiketi ya CHAN 2018 nchini Kenya, baada ya sare ya 1-1 Jumamosi mjini Mwanza.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAMUSOKO BADO ‘ANAVUTANA’ NA YANGA KUHUSU MKATABA MPYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top