• HABARI MPYA

  Monday, July 03, 2017

  CS SFAXIEN WAENDA ROBO FAINALI, ZAMALEK WAJIWEKA PAGUMU

  VIGOGO wa Tunisia, CS Sfaxien wamefuzu Robo Fainali ya kiulaini baada ya ushindi wa mabao 3-1 ugenini dhidi ya Mbabane Swallows kwenye mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Afrika uliofanyika Uwanja wa Taifa wa Somhlolo jana.
  Ndani ya nusu saa, tayari Sfaxien walikuwa mbele kwa mabao 2-0, yaliyofungwa na Ben Al Houssem na Firas Chaouat dakika ya 22 na 29.
  Karibu kabisa na mapumziko, Tshishimbi Papy Kabamba akamaliizia krosi ya Sanele Mkhweli kuwafungia wenyeji bao.
  Lakini Walid Karoui aliyetokea benchi akafunga bao la tatu dakika ya 87 na sasa washindi mara tatu, Sfaxien wanaungana na MC Alger, ambao waliifunga Platinum Stars 2-0 Ijumaa kwenda Robo Fainali.
  Katika Kundi B, mabao mawili ya kipindi cha pili ya mshambuliaji, Abbas Amidu yalitosha kuipa Caps United ushindi wa 3-1 dhidi ya Zamalek jana mjini Harare na kuzidi kufanya njia ya kwenda Robo Fainali kutoka kundi hilo iwe wazi kwa timu zote.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alifunga mabao mawili baada ya Ronald Pfumbizai kufunga la kwanza dakika ya 31 na Stanley Ohawuchi kuisawazishia Zamalek kabla ya mapumziko na kufufua matumaini ya “Makepekepe” kwenda hatua ya mtoano.
  Ushindi huo wa pili katika kundi kwa Caps unaifanya ifikishe pointi sita na kukamata nafasi ya attu, ikizidiwa pointi mbili tu na vinara, USM Alger ya Algeria na Ahly Tripoli ya Libya. Mabingwa mara tano Afrika, Zamalek wanaangukia mkiani mwa kundi wakiwa na pointi tano baada ya mechi tano.
  Caps itasafiri kwenda Algiers kuifuata USM Alger wiki ijayo, wakati Zamalek watamenyana na Ahly Tripoli mjini Cairo.

  MATOKEO KAMILI LIGI YA MABINGWA AFRIKA;
  KUNDI A
  30.06.2017    Omdurman    El Merreikh (Sudan) 2-1 El Hilal (Sudan)
  01.07.2017    Beira             Ferroviario da Beira (Mozambique) 1-1 Etoile du Sahel (Tunisia)
  KUNDI B
  30.06.2017    Sfax              Ahly Tripoli (Libya) 1-1 USM Alger (Algeria)
  02.07.2017    Harare           Caps United (Zimbabwe) 3-1 Zamalek (Egypt)
  KUNDI C
  01.07.2017    Addis Ababa   Saint George (Ethiopia) 0-1 Mamelodi Sundowns (South Africa)
  01.07.2017    Kinshasa        AS Vita (DR Congo) 2-2 Esperance (Tunisia)
  KUNDI D
  01.07.2017    Lusaka           Zanaco (Zambia) 0-0 Al Ahly (Egypt)
  01.07.2017    Garoua          Coton Sport (Cameroon) 0-2 Wydad Athletic Club (Morocco)
  KUNDI A
  02.07.2017    Kampala        KCCA (Uganda) 3-1 FUS Rabat (Morocco)
  02.07.2017    Port Harcourt Rivers United (Nigeria) 0-2 Club Africain (Tunisia)
  KUNDI B
  30.06.2017    Algiers           MC Alger (Algeria) 2-0 Platinum Stars (South Africa)
  02.07.2017    Lobamba       Mbabane Swallows (Swaziland) 1-3 CS Sfaxien (Tunisia)
  KUNDI C
  30.06.2017    Alexandria     Smouha (Egypt) 1-1 Zesco (Zambia)
  01.07.2017    El Obeid         Hilal El Obeid (Sudan) 2-0 Recreativo do Libolo (Angola)
  KUNDI D
  01.07.2017    Conakry         Horoya (Guinea) 0-0 Supersport (South Africa)
  02.07.2017    Libreville        CF Mounana (Gabon) 0-1 TP Mazembe (DR Congo)
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CS SFAXIEN WAENDA ROBO FAINALI, ZAMALEK WAJIWEKA PAGUMU Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top