• HABARI MPYA

  Monday, July 03, 2017

  MALINZI, MWESIGWA WANYIMWA DHAMANA, WARUDISHWA RUMANDE HADI JULAI 17

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi pamoja na Katibu wake, Selestine Mwesigwa na Mhasibu, Nsiande Isawafo Mwanga wamerudishwa rumande hadi Julai 17, upepelezi wa kesi yao utakapokamilika.
  Watatu hao walipandishwa tena leo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam baada ya kupelekwa rumande Julai 29, kufuatia kusomewa mashitaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti ya TFF iliyopo katika banki ya Stanbic, Dar es Salaam.
  Hakimu mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam, Wilbord Mashauri aliwanyima dhamana baada ya mabishano ya kisheria ya mawakili wa utetezi dhidi ya mawakili wa upande wa Serikali na akawapangia leo kuja tena mahakamani hapo.
  Hata hivyo, hali imeendeelea kuwa mbaya upande wa Malinzi na wenzake baada ya leo pia kunyimwa dhamana na wanarudishwa rumande.                        
  Katika mashitaka hayo, 25 yanakwenda moja kwa moja kwa Rais wa shirikisho hilo, Malinzi akidaiwa kughushi michakato mbalimbali ya kifedha, huku matatu yakiwahusu wote na Katibu wake na Mhasibu wake Nsiande Isawafo Mwanga.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MALINZI, MWESIGWA WANYIMWA DHAMANA, WARUDISHWA RUMANDE HADI JULAI 17 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top