• HABARI MPYA

  Tuesday, September 13, 2016

  ABAJALO, KARIAKOO LINDI, CDA ZAWEKWA KUNDI MOJA LIGI DARAJA LA PILI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU za Abajalo SC ya Dar es Salaam, CDA ya Dodoma na Kariakoo FC ya Lindi zimewekwa kundi moja katika Ligi Daraja la Pili Tanzania Bara.
  Timu nyingine katika kundi hilo baada ya orodha iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo, ni Changanyikeni, Cosmopolitan zote za Dar es Salaam na Burkina FC ya Morogoro.
  Kwa mujibu wa Bodi ya Ligi (TPLB), chombo maalumu cha kusimamia michezon inayoendeshwa na TFF makundi na makundi mengine ni kama ifuatavyo;
  Abajalo SC imepngwa kundi moja na CDA ya Dodoma na Kariakoo FC ya Lindi zimewekwa kundi moja katika Ligi Daraja la Pili Tanzania Bara

  Kundi A; Bulyanhulu FC (Shinyanga), Geita Gold SC (Geita), Mashujaa FC (Kigoma), Milambo SC (Tabora), Polisi Tabora FC (Tabora) na Transit Camp FC (Shinyanga). 
  Kundi B; AFC (Arusha), Green Warriors (Dar es Salaam), JKT Oljoro (Arusha), Kitayosa (Kilimanjaro), Madini SC (Arusha) na Pepsi (Arusha).
  Kundi C; Abajalo SC (Dar es Salaam), CDA (Dodoma), Changanyikeni (Dar es Salaam), Cosmopolitan (Dar es Salaam), Kariakoo FC (Lindi) na Burkina FC (Morogoro).
  Kundi D; Namungo FC (Lindi), Mawenzi Market (Morogoro), Mkamba Rangers (Morogoro), Sabasaba United (Morogoro), The Mighty Elephant (Ruvuma) na Wenda FC (Mbeya).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ABAJALO, KARIAKOO LINDI, CDA ZAWEKWA KUNDI MOJA LIGI DARAJA LA PILI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top