• HABARI MPYA

    Tuesday, September 13, 2016

    ZANZIBAR LEO IMEPIGWA 9-0 TU NA UGANDA

    Na Mwandishi Wetu, JINJA
    ZANZIBAR imepoteza mchezo wake wa pili katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Challenge) baada ya kufungwa mabao 9-0 na wenyeji Uganda leo mjini Jinja.
    Zanzibar iliyofungwa 10-1 na Burundi katika mchezo wa kwanza wa Kundi A, sasa itakamilsha mechi zake za kundi hilo kwa kumenyana na Kenya keshokutwa wakati imekwishaaga mashindano hayo.
    Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens keshokutwa inacheza mechi yake ya mwisho ya Kundi B dhidi ya Ethiopia mjini Jinja.
    Kikosi cha Zanzibar kilichofungwa 9-0 na Uganda leo Jinja
    Kilimanjaro Queens itahitaji ushindi Ijumaa ili tu kuongoza Kundi B na kupata mpinzani tahfifu kidogo katika Nusu Fainali.
    Hiyo inatokana na kwamba, Kilimanjaro Queens juzi ilijihakikishia kufuzu Nusu Fainali ya michuano hiyo baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Rwanda.
    Mabao ya Kili Queens inayofundishwa na Sebastian Nkoma, yalifungwa na Asha Rashid ‘Mwalala’ dakika za 11 na 65 na Stumai Abdallah dakika ya 28, wakati ya Rwanda yamefungwa na Ibangarrue Marie na Amina Ally wa Tanzania Bara aliyejifunga.  Rwanda na Ethiopia zitakamilisha mechi za Kundi B kwa kumenyanaa na leo.
    Nusu Fainali zitafuatia Septemba 18, kabla ya fainali kufanyika Septemba 20, 2016 ikitanguliwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ZANZIBAR LEO IMEPIGWA 9-0 TU NA UGANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top