• HABARI MPYA

  Saturday, September 24, 2016

  VITA YA KUWANIA FAINALI LIGI YA MABINGWA NI LEO

  TIMU zitakazoingia fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kuwania taji lililoachwa wazi na Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) zitajulikana leo baada ya mechi za marudiano za Nusu Fainali.
  Mamelodi Sundowns watakuwa wenyeji wa Zesco United ya Zambia Uwanja wa Lucas Moripe mjini Johannesburg, Afrika Kusini, wakati Wydad Casablanca watakuwa wenyeji wa Zamalek ya Misri Uwanja wa Complexe Prince Moulay Abdellah mjini Casablanca, Morocco.
  Katika mechi za kwanza Septemba 17, 
  Mamelodi Sundowns watakuwa wenyeji wa Zesco United ya Zambia Uwanja wa Lucas Moripe mjini Johannesburg, Afrika Kusini

  Zesco United ilishinda 2-1 dhidi ya Mamelodi Sundowns Uwanja wa Levy Mwanawasa mjini Ndola, Zambia wakati Zamalek iliifumua 4-0 Wydad Casablanca.
  Mechi za marudiano za Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Afrika zinatarajiwa kufanyika kesho, TP Mazembe ikimenyana na Etoile du Sahel Uwanja wa TP Mazembe na FUS Rabat ikimenyana na Mouloudia Olympique Bejaia ya Algeria mjini Rabat, Morocco.
  Mechi za kwanza Septemba 18, Mouloudia Bejaia ililazimishwa sare ya 0-0 na FUS Rabat Uwanja wa Unite Maghrebine mjini Bejaia, wakati Etoile du Sahel ililazimishwa sare ya 1-1 na TP Mazembe Uwanja wa Olimpiki mjini Sousse.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: VITA YA KUWANIA FAINALI LIGI YA MABINGWA NI LEO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top