• HABARI MPYA

    Monday, September 26, 2016

    FARID MUSSA AKWAMA KWENDA HISPANIA SABABU YA VISA UBALOZINI

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    KIUNGO Farid Mussa Malik amekwama kwenda Hispania kuanza maisha mapya katika klabu ya Deportivo Tenerife ya Daraja la Kwanza Hispania kutokana na kutopatiwa visa.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE leo, Farid amesema kwamba bado yuko nchini anasotea visa ya kwenda kufanya kazi Hispania.
    "Bado nipo nchini, ninasubiri visa Ubalozi wa Hispani wa hapa, kwa kweli imekuwa muda mrefu sana sasa hadi nashindwa kuelewa nini kinasababisha,"alisema Mussa.
    Azam FC imemtoa kwa mkopo Farid kwenda CD Tenerife kwa makubaliano maalum. Na hiyo ilifuatia Farid kufuzu majaribio katika klabu hiyo katikati ya mwaka alipokwenda na Mkurugenzi wa klabu yake, Yussuf Bakhresa.
    Farid Mussa (kushoto) akiwa na bosi wake, Yussuf Bakhresa walipokuwa Hispania

    Farid alitua Hispania Aprili 21 baada ya kuichezea Azam FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Esperance mjini Tunis, Tunisia ikifungwa 3-0 na kutolewa kwa jumla ya mabao 4-2 baada ya awali kushinda 2-1 Dar es Salaam.
    Na ilimchukuwa wiki moja tu Farid kuwakuna kwa kipaji chake makocha wa Tenerife na kutaka kumnunua, lakini Azam ikaktaa na kuamua kumtoa kwa mkopo.
    Azam FC haijamsajili Farid katika kikosi chake cha Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu kwa kuwa imemtoa kwa mkopo Tenerife ambayo tayari imemuombea hadi Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC). 
    Farid mwenyewe amesema amekuwa akifanya mazoezi ya peke yake tu kwa miezi miwili sasa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FARID MUSSA AKWAMA KWENDA HISPANIA SABABU YA VISA UBALOZINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top