MABINGWA watetezi, Yanga SC wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Muungano baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya wenyeji, Muembe Makumbi City usiku huu Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Mabao ya Yanga SC yamefungwa na mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo, mawili dakika ya 16 na 58, beki Mghana Kwabena Frank Assinki dakika ya 33 na kiungo Shekhan Ibrahim Khamis dakika ya 36.
Yanga SC sasa itakutana na mshindi wa Robo Fainali ya pili kesho kati ya KVZ FC na Azam FC zitakazomenyana kuanzia Saa 1:15 usiku hapo hapo Uwanja wa New Amaan Complex.
Hatua ya Robo Fainali ya michuano hiyo itakamilishwa Alhamisi kwa michezo miwili, Singida Black Stars na Mlandege FC kuanzia Saa 10:15 jioni na Simba SC dhidi ya Mafunzo kuanzia Saa 2:15 usiku hapo hapo Uwanja Amaan.
Nusu Fainali zitafuatia Aprili 25 na 26 na Fainali ya Muungano Cup 2026 itapigwa Aprili 29 mechi zote zikichezwa Uwanja wa New Alana Complex, Zanzibar.

.png)
0 comments:
Post a Comment