• HABARI MPYA

    Thursday, September 29, 2016

    WACHEZAJI WA GHANA HAWANA NGUVU KWA SABABU YA NGONO

    MKURUGENZI wa Ufundi wa klabu ya Asante Kotoko, Malik Jabir amesema wachezaji wa Ligi Kuu ya Ghana wanakosa nguvu kwa sababu wanapenda sana ngono.
    Jabir ameyasema hayo katika mahojiano maalum na Redio Ultimate FM ya Kumasi, Ghana.
    “Ngono kupita kiasi” ndiyo sababu aliyoitaja kupunguza nguvu za wachezaji Ghana.
    Kwa mujibu wa kocha huyo mkongwe, asilimia kubwa ya wachezaji wa siku hizi wanaondolewa njiani kwa urahisi na hawana uwezo wa kucheza muda wote wa mchezo kwa sababu hawalali vizuri na hawana mazoezi ya kutosha.
    “Wachezaji wengi wa leo hawawezi kucheza dakika 90, kwa sababu wanachoka haraka. Na unajua kwa nini? Kwa sababu hawalali kiasi cha kutosha na hawapati mazoezi ya kutosha na wanafanya ngono sana.”
    “Kuna wasichana wazuri wadogo Ghana Ghana na hawawezi kuwaacha peke yao,” amesema kocha Malik Jabir akizungumza na Ultimate FM na kushauri; “Kuna wakati wa hayo mambo, na wakati wa soka. Ukiyachanganya hayo mambo mawili, huwezi kufika juu,".
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WACHEZAJI WA GHANA HAWANA NGUVU KWA SABABU YA NGONO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top