Kiungo wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Kelvin Nashon ‘akisepa na kijiji cha mabeki’ wakati wa mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat - Rais wa zamani wa Congo kabla ya mchezo wa Jumapili.
Libero wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Ally Msengi (Kulia) akimiliki mpira huku Mshambuliaji wa timu hiyo, Ibrahim Abdallah akipigia hesabu mpira huo wakati wa mazoezi yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat
Beki wa kushoto wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Nickson Kibabage akimdhibiti Kelvin Nashon wakati wa mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Déba
Mshauri wa Maendeleo ya soka la Vijana, Kim Poulsen (kushoto) akimwelezea Mkuu wa Msafara wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Ayoub Nyenzi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat - Rais wa zamani wa Congo.
Muhsin Malima Makame au unaweza ukamwita ‘Super Sub’ wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, akikokota mpira kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat
Kipa Na. 1 wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Ramadhani Kabwili akifanya vitu vyake kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat
MSANIFU MKONGWE AACHA URITHI WA MAARIFA CHUO KIKUU ARDHI DAR ES SALAAM
-
*Mkuu wa Skuli ya Ubunifu Majengo, Usimamizi na Uchumi Ujenzi wa Chuo Kikuu
Ardhi (ARU), Profesa Livin Mosha akipokea sehemu ya vitabu vya usanifu
majen...
43 minutes ago
0 comments:
Post a Comment