Tovuti Hii hutembelewa na zaidi ya watu 60,000 kila siku, kutangaza biashara yako na www.binzubeiry.co.tz,
Tuma maombi kwa barua pepe 4thebetter@gmail.com.
 • HABARI MPYA

  Sunday, September 25, 2016

  MAZEMBE WATINGA FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO

  TIMU ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imefanikiwa kwenda fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya sare ya 0-0 na Etoile du Sahel ya Tunisia leo mjini Lubumbashi.
  Kwa sare hiyo ya leo kwenye mchezo wa marudiano, Mazembe inakwenda fainali kwa faida ya bao la ugenini, baada ya kutoa sare ya 1-1 ugenini katika mchezo wa kwanza.
  Mazembe yenye mshambuliaji Mtanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu sasa itakutana na mshindi kati ya FUS Rabat ya Morocco MO Bejaia ya Algeria zinazomenyana mjini Rabat usiku huu katika mchezo wa marudiano.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Note: Only a member of this blog may post a comment.

  Item Reviewed: MAZEMBE WATINGA FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top