• HABARI MPYA

  Sunday, August 14, 2016

  YANGA NJE KOMBE LA SHIRIKISHO, MEDEAMA WAIPIGA 3-2 TP MAZEMBE

  YANGA SC ya Tanzania imetupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kufuatia wenyeji Medeama SC kushinda 3-2 dhidi ya TP Mazembe ya DRC leo katika mchezo wa Kundi A Uwanja wa Essipong Sports mjini Takoradi, Ghana.
  Katika mchezo huo uliochezeshwa na Davies Ogenche Omweno aliyesaidiwa na Marwa Range wote wa Kenya na Abel Baba wa Nigeria, mabao ya Medeama yamefungwa na Enock Atta Agyei, Moses Amponsah Sarpong na Kwesi Donsu wakati ya Mazembe yote yamefungwa na Jonathan Bolingi Mpangi Merikani.
  Medeama SC sasa wameitupa nje Yanga SC Kombe la Shirikisho
  Kwa matokeo hayo, Medeama watakwenda Algeria kupigania sare kwenye mchezo wa mwisho na wenyeji Mouloudia Olympique Bejaia Agosti 23 ili kwenda Nusu Fainali, siku ambayo Yanga itakuwa ikikamilisha ratiba na TP Mazembe mjini Lubumbashi. 
  Mazembe inaendelea kuongoza Kundi A kwa pointi zake 10 baada ya mechi tano, ikishinda tatu, kufungwa moja leo na sare moja, ikifuatiwa na Medeama yenye point inane, Bejaia pointi tano na Yanga inashika mkia kwa pointi zake nne. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA NJE KOMBE LA SHIRIKISHO, MEDEAMA WAIPIGA 3-2 TP MAZEMBE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top