• HABARI MPYA

  Saturday, August 13, 2016

  YANGA KATIKA MECHI YA LAZIMA WASHINDE LEO DHIDI YA MO BEJAIA

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  MABINGWA wa mataji yote Tanzania, Yanga SC leo wanawakaribisha Mouloudia Olympique Bejaia ya Algeria katika mchezo wa marudianoa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Yanga SC inatakiwa lazima kushinda mchezo huo ili kuweka hai matumaini ya kwenda Nusu Fainali, baada ya kupoteza mechi zote tatu na mkutoa sare moja kati y azote nne za awali.
  Na pamoja na kushinda, Yanga pia itabidi iiombee dua mbaya Medeama ifungwe na TP Mazembe na baadaye ikatoe sare na Bejaia. Yanga nao watatakiwa kushinda mchezo wa mwisho dhidi ya Mazembe Lubumbashi ili kwenda Nusu Fainali.
  Kila la heri Yanga SC
  Na kwa ujumla Yanga itaingia katika mchezo wa kesho ikitoka kucheza mechi tano bila kushinda, ikiwa ni pamoja na kulazimishwa sare ya 0-0 na Mtibwa Sugar ya Morogoro katika mchezo wa kirafiki wiki iliyopita.
  Awali katika mechi zake za Kundi A Kombe la Shirikisho, ilifungwa 1-0 mara mbili, na Mouloudia Olympique Bejaia nchini Algeria na TP Mazembe Dar es Salaam kabla ya kutoa sare ya 1-1 na Medeama SC mjini hapa na baadaye kwenda kufungwa 3-1 na timu hiyo nchini Ghana katika mchezo wa marudiano.
  Mara ya mwisho Yanga kushinda ilikuwa ni kwenye Fainali ya Kombe la TFF, ilipoibugiza Azam FC 3-1 Uwanja wa Taifa. 
  Yanga itahitimisha mechi zake za Kundi A Kombe la Shirikisho kwa kumenyana na wenyeji TP Mazembe ya DRC mjini Lubumbashi Agosti 23, mwaka huu.
  Mazembe inaongoza Kundi A kwa pointi zake 10 baada ya mechi nne, ikishinda tatu na kutoa sare moja, ikifuatiwa na Bejaia na Medeama, ambazo kila moja ina pointi tano za sare tatu na ushindi mmoja, wakati Yanga inashika mkia kwa pointi yake moja. 
  Katika mchezo wa leo, Yanga itamkosa mshambuliaji wake tegemeo, Donald Ngoma ambaye atakuwa anatumikia adhabu ya kadi za njano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA KATIKA MECHI YA LAZIMA WASHINDE LEO DHIDI YA MO BEJAIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top