• HABARI MPYA

  Saturday, August 13, 2016

  MOTEAB AINUSURU AL AHLY KULALA KWA ZESCO, YATOA SARE NYUMBANI 2-2

  BAO la dakika za lala salama la Emad Moteab liliinusuru Al Ahly kufungwa nyumbani na kufanikiwa kupata sare ya 2-2 na Zesco United ya Zambia katika mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria usiku wa jana.
  Matokeo hayo yanaipeleka kileleni mwa kundi hilo Zesco wakifikisha pointi nane baada ya mechi tano, mbele ya Wydad Casablanca yenye pointi saba na leo inacheza mechi ya tano dhidi ya ASEC Mimosa ya Ivory Coast.
  Emad Moteab ameinusuru Al Ahly kufungwa nyumbani na Zesco United ya Zambia jana

  Vigogo wa Misri, Al Ahly wanapanda nafasi ya tatu kwa kufikisha pointi tano baada ya kucheza mechi tano pia, wakishinda moja, kufungwa mbili na sare mbili. 
  Mabao ya Zesco yote yalifungwa na mshambuliaji Mkenya, Jesse Were dakika za sita na 35 akimtungua kipa Ahmed Abdel wakati ya Ahly yalifungwa na Ramy Rabia dakika ya 35 na Emad Moteab dakika ya 85.
  Kikosi  cha Al Ahly kilikuwa: Adel, Fathi, Rabia, Samir, Rahil, Ashour, Ghaly, Zakaria, El-Said, Maaloul na Gamal.
  Zesco United: Banda, Silwimba, Oluwafemi, Bahn, Odhiambo, Chaila, Mtonga, Chama, Chingandu, Mwanza na Were.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MOTEAB AINUSURU AL AHLY KULALA KWA ZESCO, YATOA SARE NYUMBANI 2-2 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top