• HABARI MPYA

  Wednesday, August 17, 2016

  UONGOZI SIMBA SC WAAFIKI KUMUUZIA TIMU MO DEWJI, MCHAKATO WAANZA MARA MOJA

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  KIKAO baina ya Kamati ya Utendaji ya Simba SC na mfanyabiashara Mohamed Gulam Dewji juzi mjini Dar es Salaam kimefikia uamuzi wa kuiingiza klabu katika uendeshwaji wa mfumo wa hisa.
  Taarifa ya Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba, Hajji Sunday Manara kwa BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo imesema kwamba kikao hicho kilichofanyika hoteli ya Serena, Dar es Salaam kilikuwa muendelezo wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa klabu Julai 31.
  Manara alisema katika kikao cha juzi, Dewji aliwaeleza rasmi Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba dhamira yake ya kununua asilimia 51 ya hisa za klabu kwa Sh. Bilioni 20.
  Rais wa Simba SC, Evans Aveva (kushoto) akiwa na Bilionea kijana namba moja Afrika, Mohamed 'Mo' Dewji
  Rais huyo wa Kampuni ya Mohamed Enterprises Limited (MeTL) baada ya kuuziwa asilimia 51 ya hisa za Simba kwa Sh. Bilioni 20, ameahidi naye atawawezesha wanachama wa muda mrefu wa klabu hiyo kupewa hisa bure, ambazo wataamua wenyewe kuuza, au kununua hisa zaidi. 
  Anataka kuitoa klabu kwenye Bajeti ya Bilioni 1.2 kwa mwaka hadi Bilioni 5.5 na kwa kuamini mashabiki wa Simba wanahitaji mafanikio ya haraka, ameahidi kusajili vizuri, tuajiri kocha mzuri, ambavyo vyote vinaweza kugharimu Sh. Bilioni 4  na kwamna Bilioni 1.5 itakayobaki, ataiweka katika mradi wa ujenzi wa Uwanja.


  Mo Dewji ni mpenzi na mwanachama wa Simba SC, ambaye kati ya 1999 na 2005 alikuwa mdhamini Mkuu wa klabu na akazishawishi pia Simba Cement na NBC kuwekeza katika klabu hiyo hadi ikafuzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2003 ikiitoa Zamalek ya Misri.
  Mo pia amewahi kuwa mdhamini wa Singida United na mmiliki wa African Lyon kwa muda, kabla ya kuiuza kwa mfanyabishara Rahim ‘Zamunda’ Kangenzi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UONGOZI SIMBA SC WAAFIKI KUMUUZIA TIMU MO DEWJI, MCHAKATO WAANZA MARA MOJA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top