• HABARI MPYA

  Wednesday, August 10, 2016

  TIMU YA BURUNDI YAJA KUZIPIMA UBAVU TIMU ZA KANDA YA ZIWA

  TIMU ya Agle Noir (Black Eagles) ya Burundi leo Agosti 10, 2016 itaanza ziara ya kujiandaa na Ligi Kuu ya Burundi kwa kuweka kambi jijini Mwanza.
  Timu hii maarufu kama Tai Weusi msimu uliopita katika Ligi Kuu ya Burundi ilimaliza ikiwa ya nne kwenye msimu wa ligi nyuma ya Vital‘O na Inter Club.
  Ikiwa nchini timu hii itacheza na timu iliyopinda daraja ya Mbao FC ambayo inanolewa na Kocha Mrundi Bwana, Etienne Ndairagije na pia watacheza na Toto African na timu ya kukuza vipaji ya Alliance ya Mwanza.
  Baadaye watatembelea Shinyanga ambapo watapimana ubavu na kikosi cha Mwadui FC inayonolewa na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TIMU YA BURUNDI YAJA KUZIPIMA UBAVU TIMU ZA KANDA YA ZIWA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top