• HABARI MPYA

  Friday, August 12, 2016

  POGBA AZUIWA KUICHEZEA MAN UNITED MCHEZO WA UFUNGUZI LIGI KUU ENGLAND

  TIMU ya Manchester United itamkosa mchezaji wake iliyemsajili kwa Pauni Milioni 100, Paul Pogba katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Bournemouth Jumapili.
  Pogba amefanya mazoezi na kikosi cha kocha Mreno, Jose Mourinho leo, lakini hatasafiri kwenda Uwanja wa Vitality kwa sababu atakuwa anatumikia adhabu ya kadi.
  Chama cha Soka England (FA) kimethibitisha kwamba Mfaransa huyo alionyeshwa kadi za njano katika mechi za mwisho za Kombe la Italia, msimu uliopita. 

  Paul Pogba amefanya mazoezi na kikosi cha Jose Mourinho leo, lakini hatasafiri kwenda Uwanja wa Vitality Jumapili kwa sababu atakuwa anatumikia adhabu ya kadi za njano PICHA ZAIDI GONGA HAPA   MECHI TANO ZA MWANZO ZA MAN UTD LIGI KUU ENGLAND 

  Agosti 14: Bournemouth (ugenini)
  Agosti 19: Southampton (nyumbani)
  Agosti 27: Hull (away)
  Septemba 10: Man City (nyumbani)
  Septemba 18: Watford (ugenini) 
  Kurejea kwa Pogba katika klabu yake ya zamani, Manchester United, kulithibitishwa rasmi mapema Jumanne, lakini habari za kutocheza dhidi ya Bournemouth zinakuja kama za kushitukiza. 
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alionyeshwa kadi ya njano katika ushindi wa Juventus wa 1-0 dhidi ya AC Milan kwenye fainali ya Coppa Italia mwezi Mei, hiyo ikiwa kadi yake ya pili mfululizo kwenye mashindano hayo.
  BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE inafahamu kwamba kwa mujibu wa sheria, Pogba anapaswa kukosa mchezo mmoja baada ya kadi hizo na sasa adhabu hiyo inahamia Ligi Kuu ya England. 
  FA imesema Xherdan Shaqiri pia alikutana na mazingira hayo wakati kiungo huyo wa Uswisi alipohamia Stoke City mwaka 2015 kutoka Inter Milan
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: POGBA AZUIWA KUICHEZEA MAN UNITED MCHEZO WA UFUNGUZI LIGI KUU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top