• HABARI MPYA

    Thursday, August 11, 2016

    OFA ZA DEWJI NA MANJI SIMBA NA YANGA, NANI KALA, NANI KALIWA?

    Na Iddi Pagali, KILIMANJARO 
    WADAU kutokana na vilabu vya Yanga na Simba kuwa katika michakato tofauti  ya kuingia katika kuingia katika soka la ushindani kimataifa ni vema nitoe  maoni yangu binafsi juu ya faida na hasara za mielekeo ya – Klabu ya Yanga  Kukodisha (TIMU na NEMBO) yao kwa Mwenyekiti wao Yusuf Manji na Klabu ya  Simba kutaka kumuuzia hisa za asilimia 51 Mohamed Dewji (MO).
    Kwa kuwa sasa kuna kambi mbili na zote zina mihemko na majigambo nimeonelea  na mimi nitoe mchango wangu japo kidogo kupitia kwa ufahamu juu ya taratibu mzima na changamoto zinazozikabili vilabu vyote viwili kwa faida ya taifa letu. 
    Isije ikatokea watu wakaja kujilaumu huko mbele ya safari kuwa hawakuwa na ufahamu wa kutosha wa kile wanachokifanya sasa na kitakachoweza kutokea baadaye.
    Pia ikumbukwe kuwa haya ni maoni yangu binafsi nikiwa mdau wa mpira wa miguu nchini Tanzania:
    Mohamed Dewji anataka kununua asilimia 51 ya hisa za Simba SC kwa Sh. Bilioni 20

    1). KLABU YA SIMBA KUMUUZIA MOHAMMED DEWJI ASILIMIA 51 YA HISA ZOTE:
    a). Simba inapaswa kujigeuza na kuwa Kampuni ya Umma ya Hisa (Public Limited Company – PLC)
    b). Jumla ya Hisa ni Asilimia 100 (100%) – zenye thamani ya shilingi Bilioni 39
    c). Kama Mohemmed Dewji akiwekeza shilingi Bilioni 20 sawa na asilimia 51 (atakuwa ndiye Mwenye Hisa nyingi – Majority Shareholders). Ndiye atakayekuwa mmiliki wa Klabu na mtoa maamuzi yote yanayohusu klabu ya Simba. Kwa maana nyingine atakuwa ndiye mwenye klabu au timu
    d). Wanachama waliobakia wataambulia shilingi Bilioni 19 sawa na asilimia  
    49. Kwa kuwa kla mmoja atachukua hisa chache kulingana na uwezo wa kila  mwanachama, ina maana wote waliobaki watakuwa na Hisa Chache – Minority Shareholders. Hivyo wanachama hawatakuwa na uwezo wa aina yoyote katika  
    maamuzi ya klabu
    e). Dhana ya Simba kuwa Klabu ya Wanachama itakuwa haipo kwani itakuwa ya Wenye Hisa
    f). Pia ieleweke hapa ya kuwa kununua Hisa katika Klabu ya Simba itakuwa wazi kwa kila mtu bila kujali ni mpenzi wa Simba au siyo.
    g). Vikao vyote vitafanyika kwa mujibu wa katiba ya Kampuni chini ya Bodi  ya Wakurugenzi – Mohammed Dewji upande mmoja (Mwenye Hisa 51% - Kama Mwenyekiti na atateua watu wake atakaowaona wanafaa kuingia kwenye Bodi)   
    na Wajumbe wengine Wenye Hisa 49% watachagua wajumbe wachache kuingia kwenye Bodi.
    Lakini mwenye maamuzi ya mwisho ni Mohammed Dewji katika kila jambo.
    SWALI GUMU LA KUJIULIZA (..?..)
    Je ni kweli Klabu nzima ya Simba itakuwa na thamani isiyozidi shilingi Bilioni 39 – Jina la Klabu, Nembo, Timu, Viwanja, Majengo na Assets zake?
    MAONI YANGU: Klabu ya Simba thamani yake ni kubwa kuliko hizo shilingi  Bilioni 39. Ni wajibu wa wanasimba kufahamu hili na kufanya maamuzi ya busara katika kila hatua kwa faida yao.
    Yussuf Manji anataka kuikodisha Yanga kwa miaka 10, atakuwa anachukua asilimia 75 ya faida na 25 zitakuwa zinakwenda kwa klabu

    2). KLABU YA YANGA KUMKODISHIA YUSUF MANJI TIMU NA NEMBO KWA MIAKA 10:
    a). Yanga inabakia kuwa Klabu ya Wanachama wenye mapenzi na Yanga tu bila mabadiliko na Yusuf Manji atabakia kuwa Mwenyekiti na Kamati nzima ya  
    Utendaji
    b). Yusuf Manji akichukia Timu na Nembo kisha kuifanyia biashara kulingana na maono yake, faida zake:
    - Gharama za uendeshaji wa Klabu zitakuwa chini au hazipo
    - Klabu haitakuwa na matatizo ya aina yoyote juu ya upatikanaji wa wachezaji mahiri, malipo yao, nk kwa kuwa Yusuf Manji ndiye atakayebeba jukumu hilo
    - Klabu itakuwa ikipata mgao wake wa 25% kutokana na faida itakayopatikana pindi Manji atakapofanya biashara kupitia timu na nembo
    c). Klabu na Wanachama watakuwa huru kuingia mikataba na wabia wengine watakaojotokeza kuwekeza kwenye kuazisha Televisheni ya Yanga, Kujenga Kiwanja cha mashindano, Kujenga hosteli, nk kama atakavyofanya Yusuf Manji anapotaka kuichukua / Kuikodisha Timu na Nembo tu.
    Lakini mwenye maamuzi ya mwisho ni ya Wanachama na pengine wanachama wa Yanga watakuwa wakipata Gawio kupitia biashara zitakzokuwa zimefunguliwa na kupata faida.
    SWALI LA KUJIULIZA (..?..)
    Jina la Klabu, Nembo, Timu, Viwanja, Majengo ya Janwani na Mafia na Assets zake zina thamani gani? Ukweli Klabu inaweza ikapata thamani halisi kupitia kwa professional valuers. Lakini kiukweli thamani yake ni zaidi ya shilingi  
    Bilioni 500.
    MAONI YANGU: Klabu ya Yanga itakuwa kwenye mazingira bora na salama katika zoezi zima la kumpatia /kumkodishia Yusuf Manji Timu na Nembo alimradi pande zote mbili (Yusuf Manji na Bodi ya Udhamini) ziwe katika harakati za kusaidia Klabu ya Yanga na kuondoa dhana ya kujitajirisha katika mkataba huo.
    (Iddi Pagali ni Katibu wa Tawi la Yanga Mkoa Kilimanjaro anayepatika kwa barua pepe info@afrigalaxytours.co.tz na nambari ya simu 0766841514)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: OFA ZA DEWJI NA MANJI SIMBA NA YANGA, NANI KALA, NANI KALIWA? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top