• HABARI MPYA

  Wednesday, August 10, 2016

  NI YANGA VETERANI NA MBAGALA KUU FAINALI KOMBE LA AZAM FRESCO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  FAINALI ya Kombe la Azam Fresco itazikutanisha timu za Yanga Veterani na Mbagala Kuu Jumamosi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Hiyo inafuatia Yanga na Mbagala Kuu kuzitoa timu za Azam Veterani na TFF (Shirikisho la Soka Tanzania) katika mechi za Nusu Fainali usiku wa leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Yanga ilianza kuwatupa nje wenyeji Azam FC kwa kuwachapa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza, kabla ya Mbagala Kuu kuwafunga 1-0 TFF katika mchezo uliokuwa mkali na wa kusisimua.
  Mfungaji wa mabao yote ya Yanga Veterani leo, Gulla Joshua (kushoto) akishangilia na beki Paschal Kaliasa (kulia)

  Gulla Joshua wa Yanga Veterani (kushoto) akimtoka beki wa Azam Veterani leo

  Nahodha wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat' leo aliwekewa ulinzi mkali na Yanga 

  Mabao ya Yanga yote yalifungwa na mshambuliaji mwenye kasi ‘hadi uzeeni’ Gulla Joshua, wakati la Azam lilifungwa na Simon Lucas – na bao pekee la ushindi la Mbagala Kuu, lilifungwa na Arif Mohammed.
  Sasa TFF na Azam watakutana katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu mapema Jumamosi. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI YANGA VETERANI NA MBAGALA KUU FAINALI KOMBE LA AZAM FRESCO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top