• HABARI MPYA

  Sunday, August 21, 2016

  NIGERIA WABEBA MEDALI YA SHABA OLIMPIKI KATIKA SOKA RIO

  NIGERIA imefanikiwa kutwaa Medali ya Shaba katika michezo ya Olimpiki 2016, baada ya jana kuifunga Honduras mabao 3-2 katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu Uwanja wa Belo Horizonte, Minas Gerais.
  Shujaa wa Dream Team alikuwa ni mshambuliaji AS Roma ya Italia, Sadiq Umar aliyefunga mabao mawili dakika za 34 na 56, huku lingine likifungwa na nduguye, Aminu Umar dakika ya 49.
  Mabao ya Honduras yalifungwa na Anthony Lozano dakika ya 71 na Marcelo Pereira dakika ya 86.
  Hiyo ilikuwa Medali ya tatu kwa Nigeria kwenye Olimpiki soka kwa ujumla, baada ya mwaka 1996 kushinda Dhahabu mjini Atlanta kwa kuifunga 3-2 Argentina. 
  Timu hiyo ikafungwa na Argentina katika fainali Olimpiki ya mwaka 2008 mjini Beijing.


  Wachezaji wa Nigeria wakifurahia na Medali zao PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NIGERIA WABEBA MEDALI YA SHABA OLIMPIKI KATIKA SOKA RIO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top