WENYEJI, Singida Black Stars wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Airtel mjini Singida.
Bao pekee la Singida Black Stars katika mchezo huo limefungwa na mshambuliaji Muivory Coast, Joseph Guédé Gnadou dakika ya 71.
Kwa ushindi huo, Singida Black Stars inafikisha pointi 19 katika mchezo wa 11 na kupanda kwa nafasi mbili hadi ya tisa, wakati Coastal Union inabaki na pointi zake 15 za mechi 16 sasa nafasi ya 12.



.png)
0 comments:
Post a Comment