MUSSA HASSAN MGOSI MGUNYA ALIVYOWAAGA SIMBA SC JANA
Aliyekuwa Nahodha wa Simba, Mussa Hassan Mgosi Mgunya akipunga mkono kuwaaga mashabiki wa timu yake jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya kucheza kwa dakika tatu mechi ya kirafiki ya kumuaga dhidi ya URA ya Uganda, iliyomalizika kwa sare ya 1-1
Mgosi alipokewa familia yake iliyoongozwa na mkewe, Jasmine baada ya dakika tatu za kucheza dhidi ya URA
Hapa anatoka uwanjani kumpisha Jamal Mnyate
Hapa anasindikizwa na Shizza Kichuya kwenda nje
Hapa anamrithisha Unahodha wa timu Jonas Mkude
Hapa ni baada tu ya mchezo kusimama ili aage, akiwa ameshika mpira anapiga makofi
Hapa ni wakati anaiongoza timu kuingia uwanjani kwa mara ya mwisho kama Nahodha
Hii ndiyo familia ya Mgosi, mkewe, wanawe na mpwa wake, Amina (kushoto) aliyewahi kuwa mke wa mchezaji mwenzake wa zamani wa Simba, Athumani Machuppa
Ogun donates land to FG to develop inland dry port
-
From Idu Jude, Abuja The Government of Ogun State has donated over 130
hectares of land to the federal government of Nigeria for the development
of an in...
0 comments:
Post a Comment