• HABARI MPYA

    Monday, August 08, 2016

    HAJIB APIGA MBILI, KICHUYA MOJA, MAVUGO MOJA SIMBA SC YAITANDIKA 4-0 AFC LEOPARD

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    SIMBA SC imesherehekea vyema miaka 80 jioni ya leo baada ya kuifunga AFC Leopard ya Kenya mabao 4-0 katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Mshambuliaji chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Ibrahim Hajib Migomba ameendelea kumvutia kocha mpya, Mcameroon Joseph Marius Omog baada ya kufunga mabao mawili, huku wachezaji wapya, Mrundi Laudit Mavugo na Shizza Kichuya wakifunga pia. 
    Hadi mapumziko, Simba walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na Hajib dakika ya 38 kwa shuti la umbali wa mita takriban 30 baada ya kupokea pasi ya kiungo Mkongo, Mussa Ndusha.
    Janvier Bokungu akiwa amembeba Hajib kumpongeza baada ya kufunga. Kushoto ni mfungaji wa bao la tatu la Simba, Shizza Kichuya
    Shizza Kichuya akimtoka mchezaji wa AFC leopard leo
    Ibrahi hajib akimtoka beki wa AFC Leopars leo

    Mabadliko ya karibu nusu kikosi yaliyofanywa na kocha Omog, anayesaidiwa na Mganda, Jackson Mayanja kipindi cha pili yaliisaidia Simba kupata mabao matatu.
    Hajib alimalizia vizuri krosi ya Kichuya kuifungia Simba SC bao la pili dakika ya 56 na dakika 58 Jamal Mnyate akapoteza nafasi nzuri aliyotengenezewa na Mavungo.
    Lakini Kichuya akawainua vitini mashabiki wa Simba SC walioongozwa na Rais wa klabu, Evans Elieza Aveva na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kufunga bao la tatu dakika ya 66, akimalizia krosi ya Mavugo.
    Mavugo aliyejiunga na Simba SC mwishoni mwa wiki, akaifungia Simba SC bao la nne dakika ya 82 
    akiunganisha krosi nzuri ya Kichuya, aliyekuwa nyota wa mchezo wa leo.
    Mchezo wa leo uliokwenda sambamba na sherehe za miaka 80 ya klabu, maarufu kama Simba Day, ulihudhuriwa pia na mfanyabishara Mohammed Dewji ambaye ametoa ofa ya kuinunua klabu hiyo kwa Sh. Bilioni 20. 
    Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Vincent Angban, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Janvier Besala Bokungu/Hamad Juma dk72, Novaty Lufunga, Method Mwanjali/Juuko Murshid dk77, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto/Jamal Mnyate dk46, Mussa Ndusha/Muzamil Yassin dk46, Frederick Blagnon/Laudit Mavugo dk46, Ibrahim Hajib/Mohamed Ibrahim dk67 na Shizza Kichuya.
    AFC Leopards; Ian Otieno, Cresten Mwanzo, Bernard Mangoli, Edwin Wafula, Eugine Ambulwa, Joshua Mawira, Bernard Ongoma, Yusuf Suf Sozi, John Ndirangu, Paul Kiongera/Andrew Toloiwa dk66 na Jack Kiyai/Simon Abuko dk65.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HAJIB APIGA MBILI, KICHUYA MOJA, MAVUGO MOJA SIMBA SC YAITANDIKA 4-0 AFC LEOPARD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top