• HABARI MPYA

  Monday, January 11, 2016

  MESSI MWANASOKA BORA WA DUNIA KWA MARA YA TANO

  Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi akiwa na tuzo yake ya Ballon d'Or baada ya kukaabidhiwa usiku huu PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  WASHINDI WOTE WA USIKU WA BALLON D'OR

  Ballon d'or: Lionel Messi
  Mchezaji Bora wa Kike wa Mwaka; Carli Lloyd
  Tuzo ya Puskas: Wendell Lira
  Kocha Bora wa Kiume wa Mwaka; Luis Enrique
  Kocha Bora wa Kike wa Mwaka; Jill Ellis 
  NYOTA wa Barcelona, Muargentina Lionel Messi ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia kwa mara ya tano.
  Messi amenyakua Ballon d’Or ya FIFA akiwabwaga wapinzani wake, Mbrazil Neymar anayecheza naye Barca na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid katika hafla inayoendelea usiku huu mjini Zurich, Uswisi.
  Lionel Messi amepata asilimia 41.33 ya kura zote akifuatiwa na Cristiano Ronaldo wa Ureno aliyepata asilimia 27.76, wakati Neymar anayeingia fainali kwa mara ya kwanza, amepata asilimia 7.86.
  Mafanikio hayo yanakuja baada ya Messi kucheza mechi 53 mwaka jana akiwa na Barcelona, kufunga mabao 48 na kusababisha mabao 23, ingawa Cristiano Ronaldo alifanya vizuri zaidi, akifunga mabao 54 katika mechi 52 za Real Madrid.
  Kikosi Bora cha Dunia cha Mwaka 2015; Kutoka kushoto; Thiago Silva, Luka Modric Marcelo, Paul Pogba, Sergio Ramos, Neymar, Dani Alves, Lionel Messi, Andres Iniesta na Cristiano Ronaldo katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa usiku huu Zurich  


  WALIOWAHI KUSHINDA MARA NYINGI BALLON D'OR  

  Lionel Messi (Mara 5)
  Cristiano Ronaldo (Mara 3)
  Marco van Basten (Mara 3)
  Michel Platini (Mara 3)
  Johan Cruyff (Mara 3)
  Mchezaji mkubwa zaidi katika kizazi hiki, amepewa heshima hiyo na Manahodha wa kimataifa, makocha wa timu za taifa na Waandishi wa Habari za soka kutokana na kazi yake nzuri aliyofanya mwaka 2015, wakati Barcelona ilipoibuka timu ya kwanza kushinda mataji matatu ya ligi, Kombe na Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya pili.
  Kiwango cha Messi kilikuwa cha aina yake katika miezi 12 iliyopita, likiwemo bao lake zuri dhidi ya Bayern Munich katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa alipomchambua vizuri kipa wa dunia, Manuel Neuer kutoka umbali wa mita sita na juhudi zake binafsi katika ushindi dhidi ya Atletic Bilbao kwenye fainali ya Copa del Rey. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MESSI MWANASOKA BORA WA DUNIA KWA MARA YA TANO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top