• HABARI MPYA

  Tuesday, June 05, 2018

  YAYA TOURE AMTUHUMU PEP GUARDIOLA KUWABAGUA WACHEZAJI WA AFRIKA

  KIUNGO wa zamani wa Manchester City, Yaya Toure amemlalamikia Pep Guardiola kutopenda kuchukua wachezaji wa Kiafrika.
  Toure aliondoka Man City mwishoni mwa msimu baada ya miaka minane mizuri, lakini katika msimu wake wa mwisho hakuwa na mahusiano mazuri na Guardiola na akaanzishwa katika mechi moja tu ya Ligi Kuu England — na ya mwisho dhidi ya Brighton ambayo haikuwa na maana yoyote.
  Na sasa katika mahojiano na jarida la Ufaransa, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 mawazo yake yamempeleka mbali juu ya Guardiola na kumvisha hila za kibaguzi.

  Yaya Toure amemlalamikia Pep Guardiola kutopenda kuchukua wachezaji wa Kiafrika PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  WAAFRIKA WALIOCHEZA CHINI YA PEP GUARDIOLA

  Barcelona:
  Samuel Eto'o - Cameroon
  Seydou Keita - Mali
  Yaya Toure - Ivory Coast
  Bayern Munich:
  Medhi Benatia - Morocco
  Manchester City:
  Yaya Toure - Ivory Coast
  Kelechi Iheanacho - Nigeria 
  Akizungumza na jarida la Ufaransa, Toure alisema: "Pep anataka kuwa na wachezaji watiifu ambao wanailamba mikono yake. Sipendi uhusiano huu. Namuheshimu kocha wangu, lakini si kitu chake. Wachezaji wengine hawawezi kukubali hili hadharani, lakini baadhi tayari wameniambia waliishia kumchukia. Kwa sababu anafanya kazi na kucheza na kichwa chako,".’
  Toure amesema kwamba hakujua kabisa kwa nini hakupewa nafasi msimu uliopita kiasi cha kuwauliza makocha kwa nini hapangwi wakati alikuwa vizuri kuliko hao wachezaji chipukizi waliokuwa wanapewa nafasi. 
  "Nilihisi (Guardiola) alikuwa ana chuki, ananichukuliwa mimi kama mpinzani," alisema Toure.
  Toure ametoa mchango mkubwa kwa Man City kushinda taji la Ligi Kuu ya England mwaka 2012 na 2014, na aliisaidia pia timu hiyo kutwaa mataji ya Kombe la FA mwaka 2011 pamoja na kucheza fainali mbili za Kombe la Ligi.
  Toure alisema: "Nataka kuwa mtu aliyetoa hadithi Guardiola. Barcelona, hakufanya hivi. Alikuwa anaHe just had the akili za kufuata nyayo za Cruyf. Pep anataka kuchukuliwa mjuvi. Ninapomuona anakuna kichwa chake kuonyesha anafikiria, inanichekesha mno. ni komedi,".’
  Alipokuwa akitangaza kuondoka kwa Toure mwez Mei, Guardiola alisema: "Hii klabu imekuwa hivi ilivyo kwa sababu ya wachezaji kama Yaya. Tunashukuru kwa alivyokuwa.’
  Toure alikuwa Nahodha wa timu katika mchezo wa mwisho dhidi ya Brighton. Alikabidhiwa tiketi ya maisha na jezi iliyowekwa kwenye ngao ikiwa na namba 316, idadi ya jumla ya mechi alizocheza katika klabu hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YAYA TOURE AMTUHUMU PEP GUARDIOLA KUWABAGUA WACHEZAJI WA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top