• HABARI MPYA

  Monday, June 04, 2018

  SANE ATEMWA KIKOSI CHA MWISHO CHA UJERUMANI KOMBE LA DUNIA

  Waziri Mkuu wa Ujerumani, Angela Merkel akizungumza na wachezaji wa timu ya taifa, kutoka kushoto Leroy Sane, Julian Brandt, Leon Goretzka, Jonas Hector, Joshua Kimmich na Marc-Andre ter Stegen leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  KIKOSI CHA UJERUMANI KOMBE LA DUNIA URUSI 2018 

  Makipa: Manuel Neuer, Kevin Trapp, Marc-Andre ter Stegen.
  Mabeki: Marvin Plattenhardt, Jonas Hector, Matthias Ginter, Mats Hummels, Niklas Sule, Antonio Rudiger, Jerome Boateng, Joshua Kimmich.
  Viungo: Sami Khedira, Julian Draxler, Toni Kroos, Mesut Ozil, Sebastian Rudy, Leon Goretzka, Ilkay Gundogan.
  Washambuliaji: Marco Reus, Julian Brandt, Thomas Muller, Mario Gomez, Timo Werner. 
  NYOTA wa Manchester City, Leroy Sane ametemwa kwenye kikosi cha mwisho cha Ujerumani cha wachezaji 23 watakaocheza Fainali za Kombe la Dunia nchini Urusi.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amekuwa tegemeo la kocha Pep Guardiola na ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka PFA, lakini Joachim Low hajashawishika naye kumchukua kwenye kikosi cha kwenda kutetea Kombe Urusi.
  Sane alikuwa miongoni mwa wachezaji wachache waliokutana kwa mazungumzo na German Waziri Mkuu wa Ujerumani, Angela Merkel leo, kiasi cha saa 24 kabla hajatemwa. 
  Julian Brandt, Leon Goretzka, Jonas Hector, Joshua Kimmich na Marc-Andre ter Stegen pia walikuwemo kwenye mazungumzo hayo katika kambi ya timu nchini Italia, huko Eppan. 
  Kikosi cha Ujerumani kinachokwenda Urusi ni makipa; Manuel Neuer, Kevin Trapp, Marc-Andre ter Stegen, mabeki: Marvin Plattenhardt, Jonas Hector, Matthias Ginter, Mats Hummels, Niklas Sule, Antonio Rudiger, Jerome Boateng, Joshua Kimmich.
  Viungo; Sami Khedira, Julian Draxler, Toni Kroos, Mesut Ozil, Sebastian Rudy, Leon Goretzka, Ilkay Gundogan na washambuliaji; Marco Reus, Julian Brandt, Thomas Muller, Mario Gomez na Timo Werner.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SANE ATEMWA KIKOSI CHA MWISHO CHA UJERUMANI KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top