• HABARI MPYA

    Tuesday, August 08, 2017

    USAJILI 2017/18 WAKAMILIKA, TFF YAZISHUSHA DARAJA TIMU MBILI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    USAJILI wa timu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili kwa msimu wa 2017/18, umekamilika kwa timu 62 tu na timu mbili zimeshindwa kufanya usajili.
    Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema kwamba tayari majina ya timu husika na namna zilivyosajili, vimebandikwa katika mbao za matangazo za shirikisho hilo Uwanja wa Karume Dar es Salaam tangui.
    Taarifa hiyo imesema kwamba kubandikwa huko na kusambaza kwenye vyombo vya habari kunalenga kuwapa fursa timu zote kukagua majina ya wachezaji wa kila timu ili kuona kama kuna klabu au mchezaji amefanya udanganyifu wa kusajili wa timu zaidi ya moja, ziweze kuona,.
    Imesema kama kuna dosari hiyo, TFF imefungua milango ya kupokea pingamizi la usajili wa wachezaji hao kuanzia leo Agosti 8, 2017 hadi Jumatatu Agosti 14, mwaka huu saa 10.00 jioni (16h00).
    Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji inatarajiwa kuwa na kikao ama Agosti 16 au 17, mwaka huu kupitia mapingamizi hayo pamoja na usajili wa timu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Usajili wa timu za Daraja la Kwanza na Pili, utapitiwa baadaye mwezi huu.
    Mashabiki wa soka nchini wakae tayari kwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
    Timu hizo 62 kati ya 64 zimefanya usajili na kuingiza majina ya wachezaji, viongozi wa benchi la ufundi kwenye mfumo wa mtandao wa TMS - Transfer Matching System. 
    Lakini TFF imesema timu za Pepsi ya Arusha na Bulyanhulu ya Shinyanga zimeshindwa kufanya usajili kwa mfumo wa TMS ni za Ligi Daraja la Pili (SDL) ambazo ni.
    Na kwa msingi huo, timu hizo za Pepsi na Bulyanhulu zimejitoa kushiriki ligi kwa msimu wa 2017/18 na zinashushwa daraja hadi ligi ya wilaya kuanza upya kutafuta nafasi za juu kupanda daraja.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: USAJILI 2017/18 WAKAMILIKA, TFF YAZISHUSHA DARAJA TIMU MBILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top