• HABARI MPYA

  Sunday, August 27, 2017

  MAYWEATHER AMUADHIBU MCGREGOR 'KAMA MTOTO' ULINGONI

  Bondia Mmarekani, Floyd Mayweather Jr. akimtandika ngumi ya kidevu Conor McGregor wa Ireland katika pambano la kuwania ubingwa wa WBC uzito wa Super Welter asubuhi hii ukumbi wa T-Mobile Arena mjini Las Vegas, Marekani. Mayweather ameshinda kwa Technical Knockout (TKO) raundi ya 10 na kuweka rekodi ya kupigana mapambano 50 bila kupoteza. Mayweather alianza kwa kumsoma mpinzani wake na kumuachia atawale raundi tatu za mwanzo, lakini baada ya hapo akaanza kumchapa mfululizo hadi mwisho kama yuko mazoezini anapiga begi  PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAYWEATHER AMUADHIBU MCGREGOR 'KAMA MTOTO' ULINGONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top