• HABARI MPYA

    Friday, August 25, 2017

    RAIS FIFA AUPONGEZA UONGOZI MPYA TFF, AAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM 
    RAIS wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino, ametuma salamu za pongezi kwa uongozi mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), chini ya Rais Wallace Karia na Makamu wake, Michael Wambura.
    Rais Infantino katika barua yake ya Agosti 14, 2017 aliyoiandika kutoka Zurich, amesema: “Ningependa kuchukua nafasi hii kukupa pongezi zangu dhati. Nakutakia kila la kheri katika majukumu yako.”
    Rais wa FIFA amesema kwamba hana shaka na uwezo wa Karia hasa ikizingatiwa kuwa alikuwa Makamu wa Rais wa kipindi kilichopita, hivyo atakuwa fursa thabiti ya kuiletea nchi maendeleo ya mchezo soka.
    “Kwa wakati wote, nakuhakikishia ushirikiano wa kutosha kutoka FIFA katika malengo yako. Milango ya FIFA iko wazi wakati wowote wewe kuja kujadili masuala ya mchezo wa mpira wa miguu hasa eneo la utawala.
    “Ningependa kuchukua nafasi hii kukualika kuja hapa Zurich wakati wowote kuanzia sasa ambako nitapata  fursa ya kukutambulisha maeneo mbalimbali ya FIFA. Nimeagiza upande wa utawala kuwasiliana nawe kuona na kupanga tarehe rasmi ya safari,” amesema na kuongeza:
    “Nikutakie tena kheri na fanaka, nguvu na kila aina ya mafanikio katika majukumu yako mapya huku nikitarajia ujio wa kuonana nawe haraka.”
    Wakati huo huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu la Rwanda (FERWAFA) nalo kwa upande wake wamempongeza Rais wa TFF, Wallace Karia kwa kuchaguliwa kuwa kiongozi mpya wa shirikisho. 
    Katika barua ya FERWAFA iliyosainiwa na Rais wa shirikisho hilo, Nzamwita Vincent imesema kwamba Rwanda itaendelea kuwa bega kwa bega na Tanzania katika maendeleo ya mpira wa miguu kwa ushirikiano baina ya nchi mbili kadhalika ukanda wa Afrika Mashariki unaounda Baraza la Sola la nchi za Afrika Mashariki.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RAIS FIFA AUPONGEZA UONGOZI MPYA TFF, AAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top