• HABARI MPYA

    Friday, August 25, 2017

    VILLA AREJESHWA KIKOSINI HISPANIA BAADA YA MIAKA MITATU

    KOCHA wa Hispania, Julen Lopetegui ametaja kikosi kitakachomenyana na Italia katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia Septemba 2, mwaka huu, akimrejesha mshambuliaji mkongwe, David Villa. 
    Mshambuliaji huyo wa New York City FC, Villa aliyefunga mabao 59 ya rekodi timu ya taifa ya Hispania, alitangaza kustaafu soka ya kimataifa baada ya Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil, akifunga kwa mara ya mwisho katika mechi dhidi ya Australia, huku timu yake ikivuliwa ubingwa wa Dunia kwa kutolewa mapema tu kwenye hatua ya makundi. 
    David Villa amerejeshwa kwenye kikosi cha Hispania kwa ajili ya michezo ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Italia na Liechtenstein PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
    “Kurudishwa kwa David, wakati wote tumesema milango haijafungwa kwa yeyote na kazi yetu ni kufuatilia uchezaji wa kila mchezaji halali, na tumekuwa tukifanya hivyo wakati wote kwa David. Kwa wakati huu tunaamini uwepo wake ni kawaida na unakubalika, tunaamini atatusaidia. Amecheza vizuri katika timu yake (New York City FC) na mbali na hayo, tumeona ana ari na nia ya kutusaidia, na ndiyo maana tumemjumuisha,”  
    Julen Lopetegui kocha, alipoulizwa kuhusu Diego Costa na utayari wake kwa fainali za Kombe la Dunia Urusi, alisema;  “Kuhusu Diego Costa, vizuri, kijana amekuwa na kipindi tofauti safari hii, hafanyi hata mazoezi ya ushindani, pamoja na hayo kukosekana kwake ni kawaida, kwa sababu hizo. Baada ya hapo, tutaona kitakachotokea, acha tusibashiri chochote,”
    Costa hajajerejea kwenye klabu yake, Chelsea baada ya kuisaidia kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England msimu uliopita, kufuatia kutofautiana na kocha Mtaliano, Antoine Conte.
    Na kuhusu mshambuliaji mpya wa The Blues, Marcos Alonso, kocha Julen Lopetegui amesema;
    “Nilimuon Marcos live Wembley, lakini nimemuona mara nyingi na tunamjua vizuri sana. Anacheza misimu mizuri katika timu zenye mahitaj kama Chelsea. Lakini kwa kesi hii, tena, kuna wachezaji wengine ambao wanaweza kukidhi mahitaji yetu vizuri na kuendana vizuri na mfumo wetu wa uchezaji. Hiyo haimaanishi kwamba Marcos hawezi kuitwa hata baadaye. Mwishowe, maamuzi ya aina hiyo yanachukuliwa kutokana na vigezo vidogo,”
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: VILLA AREJESHWA KIKOSINI HISPANIA BAADA YA MIAKA MITATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top