• HABARI MPYA

    Thursday, August 24, 2017

    AZAM FC WAPO KAMILI MTWARA TAYARI KUIVAA NDANDA JUMAMOSI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIKOSI cha Azam FC jana kiliwasili salama mkoani Mtwara tayari kabisa kufungua pazi la ligi kwa kucheza na Ndanda Jumamosi Ijayo Agosti 26 mwaka huu kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
    Msafara wa Azam FC umefikia katika Hoteli ya Tiffany Diamond, iliyopo mjini Mtwara.
    Azam FC iliondoka jana mjini Dar es Salaam kwenda Mtwara, tayari kabisa kuanza rasmi msimu wa 2017-2018 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kwa kuvaana na Ndanda.
    Mchezo huo utafanyika Jumamosi wiki hii Uwanja wa Nangwanda Sijaona, ambapo kikosi hicho kimeondoka kikiwa kamili kuuanza vema msimu mpya, isipokuwa mshambuliaji Shaaban Idd, aliyeko nchini Afrika Kusini kwa matibabu ya majeraha ya misuli ya nyonga na kiungo Salmin Hoza, ambaye naye ni majeruhi.
    Msimu uliopita timu hizo zilipokutana, Ndanda ilishinda mabao 2-1 ndani ya uwanja huo, bao pekee la Azam FC ilikifungwa na mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Francisco Zekumbawira, lakini ikalipa kisasi kwa kuifunga bao 1-0 ndani ya Dimba la Azam Complex.
    Mabingwa hao wa Ngao ya Jamii na Kombe la Mapinduzi msimu uliopita, wanaodhaminiwa na Benki bora nchini ya NMB, Maji safi ya Uhai Drinking Water na Tradegents, pia msimu uliopita waliwasukuma nje Wanakuchele hao katika robo fainali ya michuano ya Kombe la FA (Azam Sports Federation Cup) kwa kuwanyuka mabao 3-1. mabao mawili yakifungwa na Shaaban Idd na jingine likiwekwa kimiani na Ramadhan Singano 'Messi'.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC WAPO KAMILI MTWARA TAYARI KUIVAA NDANDA JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top