• HABARI MPYA

    Monday, August 28, 2017

    MAPEMA TU, TFF WABOMOA RATIBA YA LIGI KUU

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    BODI ya Ligi (TPLB) ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limefanya mabadiliko kidogo katika michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kama ifuatavyo.
    Michezo ambayo imefanyiwa mabadiliko ni kati ya Tanzania Prisons na Majimaji ya Songea; Azam FC na Simba, Njombe Mji na Yanga SC; Mtibwa Sugar na Mwadui FC ambayo sasa itachezwa Septemba 6, 2017.
    "Pia tarehe hiyo ya Septemba 6, mwaka huu kutakuwa na mechi kati ya Lipuli na Stand United; Singida United na Mbao; Kagera Sugar na Ruvu Shooting wakati Mbeya City na Ndanda FC .
    Mechi ya mwisho ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ilimalizika kwa sare ya 1-1 kati ya wenyeji, Yanga na Lipuli ya Iringa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam jana  
    Michezo mingine ambayo imesogezwa hadi Septemba 11, 2017 ni kati ya Azam na Kagera Sugar wakati Mbao na Tanzania Prisons utachezwa Septemba 21, mwaka huu.
    Kadhalika mechi nyingine zitachezwa Oktoba 11, mwaka huu ni kati ya Mbao na Azam FC; Kagera Sugar na Mwadui; Mbeya City na Ruvu Shooting; Ndanda na Singida United.
    Tarehe hiyo pia Oktoba 11, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Njombe Mji na Simba; Mtibwa na Tanzania Prisons; Lipuli na Majimaji wakati Stand United na Young Africans watacheza Oktoba 12, mwaka huu.
    Novemba 15, 2017 Mbao itacheza na Young Africans; Kagera na Mbeya City; Stand United na Azam; Mwadui na Ruvu Shooting; Singida na Njombe Mji; Lipuli na Tanzania Prisons; Mtibwa Sugar na Majimaji wakati Novemba 16, Ndanda itacheza na Simba. Mabadiliko hayo yanakuja baada ya Ligi Kuu kuchezwa kwa raundi moja tu mwishoni mwa wiki.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAPEMA TU, TFF WABOMOA RATIBA YA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top