• HABARI MPYA

    Saturday, August 26, 2017

    OKWI AITWA KUIBEBA UGANDA KUFUZU KOMBE LA DUNIA

    KOCHA wa muda wa Uganda, Moses Basena amemjumuisha mshambuliaji mpya wa Simba SC ya Tanzania, Emmanuel Okwi kwenye kikosi cha awali cha wachezaji 27 kwa ajili ya michezo miwili mfululizo ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Misri.
    The Cranes watakuwa wenyeji wa Mafarao kwenye mchezo wa Kundi E Agosti 31 mjini Kampala kabla ya kusafiri siku tano baadaye kwenda mjini Alexandria kwa mchezo marudiano.
    Kuna wachezaji kadhaa wamerejeshwa kikosini akiwemo beki, Isaac Isinde anayechezea Buildcon ya Zambia, kiungo William Luwagga Kizito wa CSM Politehnica Iași ya Romania na kiungo wa ulinzi, Ivan ‘Kojja’ Ntege, ambaye hivi karibuni amejiunga na mabingwa wa Botswana, Township Rollers.
    Luwagga aligomea wito wa kocha aliyeondoka, Mserbia Milutin ‘Micho’ Sredejovic, lakini Basena ameamua kumpa nafasi ya pili.
    Emmanuel Okwi ameitwa kwenye kikosi cha Uganda kwenye michezo miwili mfululizo ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Misri

    The Cranes ina pointi nne baada ya mechi mbili, ikiwa nyuma ya vinara, Misri. Ghana na Kongo zinafuatia katika nafasi ya tatu na ya nne mpja ikiwa na pointi moja na nyingine haina pointi.
    Uganda wanataraji kufuzu kwa mara ya kwanza kwenye Kombe la Dunia tangu lilipoanzishwa mwaka 1930.
    Kikosi kamili cha awali cha Uganda kinaundwa na makipa: Dennis Onyango (Mamelodi Sundowns, Afrika Kusini), Robert Odongkara (St George, Ethiopia), Ismail Watenga (Vipers) na Benjamin Ochan (KCCA).
    Mabeki ni; : Nico Wakiro Wadada (Vipers), Isaac Muleme (KCCA), Timothy Dennis Awany (KCCA),Juuko (Simba, Tanzania), Bernard Muwanga (SC Villa), Geofrey Walusimbi (Gor Mahia, Kenya), Dennis Iguma (Al Ahed, Lebanon), Paul Musamali (KCCA), Isaac Isinde (Buildcon, Zambia)
    Viunggo ni: William Luwagga Kizito (CSM Politehnica Iași, Romania), Aucho Khalid (huru), Geofrey ‘Baba’ Kizito (Than Quảng Ninh, Vietnam), Ivan Ntege (Township Rollers, Botswana), Muzamiru Mutyaba (KCCA), Moses Waiswa (Vipers), Shafiq Kagimu (URA), Wasswa Hassan Mawanda (Njimeh Lebanon), Joseph Ochaya (Lusaka Dynamos, Zambia)
    Washambuliaji: Derrick Nsibambi (KCCA), Geofrey Sserunkuma (Buildcon, Zambia), Emmanuel Okwi (Simba, Tanzania), Milton Karisa (Vipers), Faruku Miya (Standard Liege, Ubelgiji)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: OKWI AITWA KUIBEBA UGANDA KUFUZU KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top