• HABARI MPYA

    Thursday, August 31, 2017

    NYOTA WA URENO AKWAMA KUJA KUJIUNGA NA TAIFA STARS

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI Orgenes Mollel (pichani kulia) wa FC Famalicao ya Ureno hataweza kuja kujiunga na kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa ajili ya mchezo dhidi ya Botswana Jumamosi Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. 
    Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas sababu za Mollel kushindwa kuja kutopata ruhusa. "Taratibu za ruhusa za kimataifa zinafanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria za nchi ya Ureno ambako anacheza soka la kulipwa,"amesema Lucas.
    Nyota wengine wanaocheza nje wamekwisharipoti ambao ni Nahodha Mbwana Samatta wa KRC Genk ya Ubelgiji, Elias Maguli wa Dhofar FC ya Oman, Abdi Banda wa Baroka FC ya Afrika Kusini, Hamisi Abdallah wa Sony Sugar ya Kenya, wakati Farid Mussa wa CD Tenerife ya Hispania anatarajiwa kutua leo.
    Tayari TFF leo imetangaza viingilio vya mchezo huo ambavyo vitakuwa ni Sh 10,000 kwa Jukwaa Kuu na Sh 5,000 kwa mzunguko.
    Kikosi kamili cha Stars kilichopoa kambini Hoteli ya Sea Scape, Kunduchi, Dar es Salaam ni makipa Aishi Manula (Simba SC), Mwadini Ally (Azam FC) na Ramadhani Kabwili (Young Africans).
    Mabeki; Gardiel Michael (Yanga SC), Boniphas Maganga (Mbao FC), Kelvin Yondani (Yanga SC), Salim Mbonde (Simba SC) na Erasto Nyoni (Simba SC).
    Viungo ni Himid Mao - Nahodha Msaidizi (Azam FC), Mzamiru Yassin (Simba SC), Said Ndemla (Simba SC), Shiza Kichuya (Simba SC), wakati Washambuliaji ni Raphael Daud (Yanga SC), Kelvin Sabato (Azam FC) na Emmanuel Martin (Yanga SC).
    Katika hatua nyingine, Botswana inatarajiwa kuingia usiku wa saa 3.00 kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (KQ) na watafikia Hoteli ya Urban Rose iliyoko katikati ya jiji la Dar es Salaam.
    Botswana inayonolewa na David Bright inakuja na wachezaji 18 wakiwamo makipa Mampule masule, Noah Maposa na Antony Gouws.
    Walinzi ni Letsweletse, Mosha Gaolaolwe, Simisane Mathumo, Thabang Mosigi, Lesenya Ramorake, Tapiwa Gadibolae na Bokani Leeton.
    Viungo ni Alphonse Modisaotsile, Maano Ditshupo, Katlego Masole, Gift Moyo, Segolame Boy, Lemponye Tshireletso, Thero Setsile, Kabelo Seakanyeng,Jackson, Lemogang maswena.
    Washambuliaji ni Tumisang Orebonye, Jarome Ramathakwane, Tebogo Sembowa, Hendric Moyo na Boipelo Oaitse.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NYOTA WA URENO AKWAMA KUJA KUJIUNGA NA TAIFA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top