• HABARI MPYA

    Wednesday, August 23, 2017

    KOCHA RAYON ATAMBA KUFANYA KWELI LIGI YA RWANDA

    Na Canisius Kagabo, KIGALI
    KOCHA wa Rayon Sports, Karekezi Olivier amethibitisha kikosi cha timu yake cha wachezaji 25 anapaswa kutumia msimu huu kwa ligi kuu ya Rwanda 'azam Rwanda Premier League'.
    Tangu tarehe 25 Julai timu hii ilianza mazoezi kwa kujitayalisha msimu wa 2017/2018. Walicheza mchezo wa kirafiki na Simba SC ya Tanzania wakashindwa na timu hii 1-0.
    Baada ya mchezo huu Karekezi aliendelea na mazoezi na wachezaji wote kufika idadi ya 37, jana jioni alifanya mkutano na wasaidizi wake kwa kuwachaguwa wachezaji 25 bora kuliko wengine atatumia msimu huu.
    Kocha Olivier Karekezi (kulia) akiwa kazini na timu yake, Rayon Sports 
    Akizungumuza na vyombo vya habari Karekezi amesema kwamba anawahitaji wachezaji 25 tu lakini mwezi Januari anaweza kumsajiri mchezaji mmoja wa kumusaidia kwa mashindano ya CAF.
    "Tutabaki na wachezaji 25 tu, ndio napanga kutumia msimu huu kwa ligi, vinawezekana kwamba Januari nitamsajirisha mwingine wa kunisaidia kwenye mashindano ya CAF(CAF champions League). 
    Timu hii kabla ya ligi kuanza inapanga kucheza michezo mitatu ya kirafiki, miwili itachezwa mwishoni wiki hii, AS Muhanga na Amagaju FC timu za Rwanda, mwingine watakutana na Villa ya Uganda tarehe 2 Septemba.
    Listi kamili ya wachezaji 25 Rayon Sports msimu huu; Kipa: Ndayishimiye Eric Bakame(Rwanda), Mutuyimana Evariste (Rwanda)na Kasim(Rwanda)
    Mabeki: Manzi Thierry(Rwanda), Usengimana Faustin(Rwanda), Rwatubyaye Abdoul(Rwanda), Mutsinzi Ange(Rwanda), Mugabo Gabriel(Rwanda), Irambona Eric(Rwanda), Nzayisenga Jean d’Amour (Rwanda), Mugisha François(Rwanda, Rutanga Eric(Rwanda), Nyandwi Sadam(Rwanda)
    Viungo :Kwizera Pierrot(Burundi), Niyonzima Olivier Sefu(Rwanda), Niyonzima Ally(Rwanda), Muhire Kevin(Rwanda), Nova Bayama(Rwanda), Manishimwe Djabel(Rwanda), Habimana Yussuf(Rwanda)
    Washambuliaji:Tediane Kone(Mali), Bimenyimana Caleb Bonfils(Burundi), Nahimana Shassir(Burundi), Arasane Tamboura(Mali) na Mugisha Gilbert(Rwanda).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KOCHA RAYON ATAMBA KUFANYA KWELI LIGI YA RWANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top