• HABARI MPYA

    Friday, August 25, 2017

    VAN PERSIE AREJESHWA KIKOSINI UHOLANZI BAADA YA MIAKA MIWILI

    Mkongwe Robin van Persie amerejeshwa kikosini Uholanzi kwa ajili ya michezo ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Ufaransa na Bulgaria PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

    KIKOSI KAMILI CHA UHOLANZI

    MAKIPA: Jaspen Cillessen, Maarten Stekelenburg, Jeroen Zoet
    MABEKI: Nathan Ake, Daley Blind, Wesley Hoedt, Matthijs de Ligt, Karim Rekik, Kenny Tete, Joel Veltman, Stefan de Vrij
    VIUNGO: Donny van de Beek, Marco van Ginkel, Tonny Vilhena, Davy Propper, Wesley Sneijder, Kevin Strootman, Gini Wijnaldum
    WASHAMBULIAJI: Vincent Janssen, Robin van Persie, Quincy Promes, Arjen Robben, Bas Dost, Memphis Depay
    KOCHA wa Uholanzi, Dick Advocaat amemrejesha kikosini  mshambuliaji mkongwe, Robin van Persie kwa ajili ya michezo migumu wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Ufaransa na Bulgaria.
    Mshambuliaji wa Fenerbahce, Van Persie alicheza mechi yake ya mwisho na ya 101 ya kimataifa Oktoba mwaka 2015. 
    Mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal na Manchester United mwenye umri wa miaka 34 ndiye anayeongoza kwa ufungaji katika timu yake ya taifa, akiwa amefunga mabao 50 na sasa Uholanzi inamhitaji tena kikosini kurejea kuzisaka nyavu. 
    Baada ya mechi sita, Uholanzi inashika nafasi ya tatu katika Kundi A, ikizidiwa pointi tatu na vinara, Sweden, wanaoongoza kundi hilo kwa wastani wa mabao dhidi ya Ufaransa. Ni mshindi wa kundi pekee anayejihakikishia nafasi ya kwenda Kombe la Dunia la Urusi.
    Mchezaji anayetakiwa na Liverpool, Virgil van Dijk, ambaye hajacheza hata mechi moja Southampton msimu huu akilazimisha kuondoka, hajaitwa.
    Uholanzi itacheza na Ufaransa Alhamisi mjini Saint-Denis kabla ya kurudi Amsterdam kumenyana na Bulgaria Septemba 3.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: VAN PERSIE AREJESHWA KIKOSINI UHOLANZI BAADA YA MIAKA MIWILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top