• HABARI MPYA

    Tuesday, August 29, 2017

    HATIMA YA CHIRWA WA YANGA KUJULIKANA KESHO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), chini ya Mwenyekiti wake Tarimba Abbas, inatarajiwa kuketi kesho Jumatato Agosti 30, mwaka huu.
    Kamati hiyo itakuwa na ajenda kadhaa ikiwamo ya mashauri yanayohusu wachezaji mbalimbali, viongozi na klabu.
    Shauri mojawapo linahusu ripoti ya Mechi namba 236 ya Ligi Kuu ya Vodacom uliokutanisha timu za Mbao FC na Yanga uliofanyika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Yanga ikipoteza kwa bao 1-0.
    Mara baada ya mchezo huo, Kamati ya 72 ya Bodi ya Ligi ilipitia matukio mbalimbali na kufikia uamuzi wa kuwasimamisha wachezaji Deus Kaseke, Simon Msuva na Obrey Chirwa wa Yanga kucheza mechi za Ligi Kuu.
    Hatima ya nyota Mzambia wa Yanga, Obrey Chirwa inatarajiwa kujulikana Jumatano mbele ya Kamati ya Nidhamu ya TFF 
    Walisimamishwa wakisubiri suala lao la kumsukuma na kumwangusha Mwamuzi Ludovic Charles kusikilizwa na kutolewa uamuzi na Kamati ya Nidhamu ya TFF.
    Wachezaji hao walidaiwa kufanya kitendo hicho katika mechi hiyo dhidi ya Mbao FC iliyofanyika Mei 20, 2017 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijni Mwanza. Uamuzi wa Kamati ya Saa 72 ulizingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu.
    Mwamuzi Ludovic Charles amepewa onyo kali kwa kutodhibiti vizuri mchezo. Uamuzi dhidi yake ni kwa mujibu w Kanuni ya 38(5) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HATIMA YA CHIRWA WA YANGA KUJULIKANA KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top