• HABARI MPYA

  Tuesday, August 08, 2017

  OMOG AMUANZISHIA BENCHI NIYONZIMA MECHI NA RAYON LEO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mcameroon, Joseph Marius Omog amemuanzishia benchi kiungo mpya, Haruna Niyonzima katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Rayon Sport unaotarajiwa kuanza Saa 10:00 jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Simba wanawakaribisha mabingwa wa Ligi Kuu ya Rwanda katika mchezo wa kuhitimisha tamasha la Simba Day leo, ambalo ni maalum kutambulisha kikosi na jezi za msimu mpya za washindi hao wa Azam Sports Federation Cup (ASFC), michuano ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

  Haruna Niyonzima anaanzia benchi leo katika mchezo na Rayon Sport unaotarajiwa kuanza Saa 10:00 jioni  

  Na katika mchezo huo, kocha Omog anayesaidiwa na Mganda, Jackson Mayanja hajamuanzisha pia mshambuliaji mpya kutoka Ghana, Nicholas Agyei.
  Kikosi kitakachoanza dhidi ya Rayon Sports leo ni Aishi Manula, Erasto Nyoni, Jamal Mwambeleko, Method Mwanjali, Salim Mbonde, James Kotei, Shiza Kichuya Muzamil Yassin, John Bocco, Emmanuel Okwi na Mohammed ‘Mo’ Ibrahim.
  Maana yake katika benchi watakuwapo Said Mohammed, Eamanuel Mseja, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Yussuf Mlipili, Ally Shomary, Jonas Mkude, Said Ndemla, Mwinyi Kazimoto, Haruna Niyonzima, Jamal Mnyate, Laudit Mavugo, Nicholas Gyan. 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: OMOG AMUANZISHIA BENCHI NIYONZIMA MECHI NA RAYON LEO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top