• HABARI MPYA

    Tuesday, August 01, 2017

    UCHAGUZI MKUU TAFCA AGOSTI 10, JULIO ATATOKA?

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    UCHAGUZI Mkuu wa Chama cha Makocha wa Soka Tanzania (TAFCA utafanyika Agosti 10, mwaka huu mjini Dodoma.
    Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA, Ramadhani Mambosasa ametangaza orodha ya majina sita ya mwisho ya wagombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo.
    Kwa mujibu Mambosasa, wagombea hao kwa sasa hawana budi kuendelea na kampeni hadi Agosti 9, mwaka huu.
    Waliopitishwa katika orodha ya mwisho kuwania nafasi mbalimbali za uongozi - ngazi ya taifa ni pamoja na Kidao Wilfred, Lister Manyara, Michael Bundala, Dismas Haonga, Jamhuri Kihwelo, George Komba, Samuel Moja na Maka Mwalwasi na Mohammed Tajdin.
    Nafasi zinazowaniwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina, Wajumbe wa Mkutano Mkuu TFF na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UCHAGUZI MKUU TAFCA AGOSTI 10, JULIO ATATOKA? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top