• HABARI MPYA

    Saturday, August 12, 2017

    NANI KURITHI KITI CHA MALINZI TFF LEO?

    Na Mwandishi Wetu, DODOMA
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) leo linatarajiwa kupata viongozi wapya katika uchaguzi utakaofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa jengo la St. Gasper mjini Dodoma.
    Kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu, nafasi za juu zina ushindani mkali na hadi kuelekea siku ya kupiga kura hakuna hata dalili za nani anaweza kushinda.
    Wagombea wa nafasi ya Urais ni Kaimu Rais wa sasa, Wallace Karia, anayechuana na mchezaji wa zamani wa timu ya taifa, Ally Mayay, Katibu wa zamani wa shirikisho hilo, Frederick Mwakalebela, Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Yanga, Wakili Imani Madega, Msomi na Mwandishi wa Habari za Michezo wa zamani, Shija Richard na Katibu wa klabu ya Mbeya City, Emmanuel Kimbe.
    Katika nafasi ya Umakamu wa Rais Mwenyekiti wa FA ya Dodoma, Mulamu Nghambi anachuana na Katibu wa zamani wa TFF, Michael Wambura, mchezaji wa zamani wa timu ya taifa, Mtemi Ramadhani, Robert Selasela na Stephen Mwakibolwa.
    Rais wa TFF, Jamal Malinzi (katikati) ameshindwa kurudi kutetea nafasi yake baada ya kuweka rumande tangu Juni 29

    Uchaguzi huu umekuwa mzito kutokana na Serikali kupitia Taasisi zake mbalimbali ikiwemo ile ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kuumulika kuhakikisha wagombea hawatumii njia zisizo halali kuwashawishi wapiga kura.
    Ikumbukwe aliyekuwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi ameshindwa kurudi kutetea nafasi yake baada ya kuweka rumande tangu Juni 29, mwaka huu kwa pamoja na Katibu weke, Selestine Mwesigwa na Isinde Isawafo Mwanga kwa tuhuma za ubadhirifu.
    Watatu hao walipelekwa rumande Juni 29 baada ya kusomewa mashitaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti ya TFF iliyopo katika banki ya Stanbic, Dar es Salaam.
    Katika mashitaka hayo, 25 yanakwenda moja kwa moja kwa Rais wa shirikisho hilo, Malinzi akidaiwa kughushi michakato mbalimbali ya kifedha, huku matatu yakiwahusu wote na Katibu wake na Mhasibu wake Nsiande Isawafo Mwanga.
    Malinzi aliingia madarakani TFF Oktoba mwaka 2013 baada ya kupata kura 72 kati ya 126 zilizopigwa akimshinda aliyekuwa mpinzani wake wa karibu, Athumani Nyamlani, lakini baada ya kesi hiyo kuanza kuunguurma na kuwekwa rumande, Kamati ya Utendaji ya TFF ilikutana na kumteua Makamu wake, Wallace Karia kukaimu Urais wa shirikisho hilo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NANI KURITHI KITI CHA MALINZI TFF LEO? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top