• HABARI MPYA

  Thursday, July 20, 2017

  YANGA KUMUUZA MSUVA MILIONI 300 MOROCCO, KILA KITU SAFI BADO VIPIMO VYA AFYA TU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WINGA wa Yanga SC, Simon Msuva atakwenda Morocco wiki ijayo kufanya vipimo vya afya katika mpango wa kujiunga na klabu ya Ligi Kuu nchini humo, Difaa Hassani El-Jadida kwa ada ya uhamisho ya dola za Kimarekani 150,000 zaidi ya Sh Milioni 300 za Tanzania.
  Difaa ambayo tayari imekwishamchukua Mtanzania mwingine, winga pia Ramadhani Singano ‘Messi’ kutoka Azam FC iko tayari kutoa dola 150,000 kumnunua Msuva ambaye amebakiza miezi tisa katika mkataba wake Yanga.
  Msuva alishindwa kuondoka jana kwenda Kigali, Rwanda na kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars kwa ajili ya mchezo wa marudiano Raundi ya kwanza kuwania tiketi ya Faianli za Ubingwa wa Mataifa wa Afrika (CHAN), zinazohusisha wachezaji wanaocheza nchini mwao pekee, ili kushughulikia safari yake Morocco.
  Simon Msuva atakwenda Morocco wiki ijayo kufanya vipimo vya afya kuelekea uhamisho wake wa dola 150,000 kwenda Difaa Hassani El-Jadida 

  Na baada ya kukamilisha taratibu zote, Msuva ameondoka leo Dar es Salaam kwenda Kigali kuungana na Stars kujaribu kupata matokeo mazuri ugenini baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza Mwanza Jumamosi.
  Baada ya mchezo na Amavubi mjini Kigali Jumamosi, Msuva aliyejiunga na Yanga mwaka 2012 kutoka Moro United, anatarajiwa kwenda moja kwa moja Morocco kwa ajili ya vipimo vya afya ambavyo akifuzu atasaini mkataba mnono.
  Timu hiyo yenye maskani yake mji wa El Jadida ikiwa inatumia Uwanja wa El Abdi inataka kujaribu kutwaa taji la Ligi Kuu ya Morocco, inayojulikana kama Botola, moja ya Ligi bora kabisa barani Afrika.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA KUMUUZA MSUVA MILIONI 300 MOROCCO, KILA KITU SAFI BADO VIPIMO VYA AFYA TU Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top