• HABARI MPYA

  Friday, July 21, 2017

  TIMU 24 SASA KUCHEZA FAINALI ZA AFCON JUNI NA JULAI

  FAINALI za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) sasa zitakuwa zikifanyika katikati ya mwaka badala ya mwanzoni na idadi ya timu za kushiriki zinaongezeka hadi 24 kutoka 16.
  Michuano hiyo kuhamishwa kutoka Januari na Februari hadi Juni na Julai kuanzia Fainali za mwaka 2019 nchini Cameroon ni habari njema kwa makocha wa Ligi Kuu ya England na Ulaya kwa ujumla. 
  Makocha wa England na Ulaya kwa ujumla wamekuwa wakiichukia michuano ya AFCON kwa sababu hufanyika kipindi ambacho Ligi zao zimeshika kasi na wachezaji wao tegemeo wa Kiafrika hulazimika kurejea nyumbani.

  Mabingwa wa Afrika, cameroon wakisherehekea na taji lao mapema mwaka huu Gabon PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  Lakini CAF imesema michuano hiyo itaendelea kufanyika kila baada ya miaka miwili na itaendelea kufanyika katika ardhi ya Afrika.
  Katika AFCON ya mwaka huu ambayo Cameroon waoiibuka mabingwa nchini Gabon, wachezaji 21 wa Ligi Kuu ya England kutoka klabu 12 tofauti walishiriki.
  Sunderland, Stoke na Leicester ndiyo waliokuwa na wachezaji wengi zaidi.
  Mabadiliko haya yamefanyika katika Mkutano wa Kamati Kuu ya CAF uliofanyika mjini Rabat, Morocco Alhamisi. 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TIMU 24 SASA KUCHEZA FAINALI ZA AFCON JUNI NA JULAI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top