• HABARI MPYA

  Thursday, July 20, 2017

  MTIBWA SUGAR WAMREJESHA KADO KUZIBA PENGO LA MDUDA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIPA wa Mwadui FC, Shaaban Hassan Kado leo amesaini mkataba wa miaka miwili kurejea timu yake ya zamani, Mtibwa Sugar ya Morogoro. 
  Mtibwa Sugar wanamrejesha Kado baada ya aliyekuwa kipa wa kwanza wa timu hiyo, Said Mohammed Mduda kusaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Simba SC. 
  Kado mwenye umri wa miaka 28, anarejea Mtibwa Sugar baada ya kuondoka Desemba mwaka 2012 kuhamia Coatsal Union ya Tanga, aliyoidakia hadi mwaka juzi alipokwenda Mwadui FC ya Shinyanga.
  Shaaban Kado leo amesaini mkataba wa miaka miwili kurejea timu yake ya zamani, Mtibwa Sugar ya Morogoro 

  Kado anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa Mtibwa Sugar katika dirisha hili, baada ya Hussein Idd kutoka JKT Oljoro, Suleiman Kihimbi kutoka Polisi Morogoro na Salum Kanoni kutoka Mwadui FC pia.
  Na anakwenda kuwa kipa namba moja tena Mtibwa Sugar mbele ya Benedictor Tinocco na Abdallah Makangana ‘Dida’.
  Kado aliyetimiza umri wa miaka 28 Aprili 14, mwaka huu alisajiliwa Mtibwa Sugar kwa mara ya kwanza kabisa mwaka Julai 1, mwaka 2008 akitokea Moro United, ya Morogoro pia na akadumu hadi Mei mwaka 2011 alipohamia Yanga SC ambako alidumu kwa msimu mmoja tu na kurejeshwa Manungu kwa mkopo.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR WAMREJESHA KADO KUZIBA PENGO LA MDUDA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top